January 06, 2020

Wananchi Karatu walia na bei kubwa ya maji!

Ofisi za Maji Karatu (KARUWASU).
Na Bryceson Mathias, Karatu
WANANCHI wasio na uwezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mjini mkoani Arusha, wameilalamikia Serikali kuu wakidai, wamelia kwa muda mrefu kwamba wanaumizwa na bei kubwa ya Maji ya Shs. 3,000/- kwa ‘Unit’, hivyo wanaomba iwasaidie.
Wakihojiwa na Mwandishi kwa Nyakati tofauti Wanyonge hao wamedai, wamechoshwa kununua ‘’Unit’ moja ya Maji kwa Shs. 3,000/- kwa kuwa bei hivo sasa imekuwa kama msumari wa moto, wakitaka Serikali ikamilishe Mradi wake wa Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority (AUWSA) ili wafute makovu.
Aidha wamedai, baadhi ya wananchi waliyopata bahati ya kutumia maji yanayotolewa na Taasisi ya Serikali ya Karatu Rural Water Supply (KARUWASU) wanafaidi matunda ya Wananchi kwa sababu Unit Moja yenye Ndoo 50 zenye Lita 20 wananunua Shs. 1,750/-.
Wamelia wakisema, unapokinga maji yake unapata maji halisi hakuna gesi lakini kwenye maji wanayouziwa Tzs. 3,000/- kwa Unit kwanza unaanza kupa hewa ikifoka halafu baadaye ndiyo unapata maji jambo ambao linaongeza gharama kwao.
Kutokana na gharama hiyo na wengine kuambulisha hewa (pesure) kabla ya maji, wameamua kuacha na kulazimika kununua maji yanyouzwa kwenye kwa Shs. 2,000/- kwa DUMU ambapo wanaona ni nafuu zaidi.
Kaimu Meneja wa KARUWASU, Jackson Njau, alipoulizwa wana mpango gani wa kusambaza huduma yao Karatu yote kama itikio la kusikiliza kilio cha wananchi wanyonge dhidi ya bei kubwa ya Maji alisema,
“Ninawaomba wananchi wawe wavumilivu wakati wanakamilisha juhudi za kukamilisha Kufunga Pumpu kwenye Kisima kilichoko kwenye eneo ulipokuwepo Mti wa wapendao na Ishalah mambo yakienda sawia huduma yao itakuwa imesambaa Karatu nzima”.alisema Njau aliyekiri gharama ya bei ya maji wanayoipata wananchi wanaifahamu.
Mmoja wa watendaji wa Maji Karatu Mjini na Vijijini (KAVIWASU), anayeshughulika na huduma aliyejitambulisha kwa jina moja la Emma alisema, bei ya Maji yao si Tzs. 3,000/- kwa Unit pekee! Bali kuna Tzs. 2,000/- kulingana na mahali ambapo maeneo ya mjini bei ni kubwa kama ilivyotajwa na vijijini ni ndogo.
Aliyekuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, alipowahi kutembelea tanki kubwa la kusambaza maji Karatu ambalo kwa wakati huo lilikuwa na uwezo wa kusambaza zaidi ya lita 30,000 kwa saa, aliwahi kutoa uamuzi wilayani humo akisema,
“Ingawa kuna Bodi ya Maji Karatu Mjini na Vijijini (KAVIWASU), bado kuna haja ya kuundwa chombo kipya ambacho kinaweza kuunganishwa na KAVIWASU ili kuongeza uwazi”.alisema Pinda ambapo Serikali ilitangaza mpango wa kuunda Mamlaka ya Maji Karatu ili kusimamia usambazaji wa huduma hiyo wilayani humo.
Wakati huo huo Januari, 2019 mwaka jana, Naibu Waziri wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) aliwahi kumtaka Mkuu wa wilaya ya Karatu, Theresia Mahongo,  kuwatafuta wataalam wa Serikali, pamoja na wakandarasi waliopata zabuni za kutekeleza miradi ya maji wilayani humo kufika wilayani bila kukosa ndani ya siku 14.
Wito huo ulikuwa ni kuanzia 28 Januari, 2019 ili kufanyika kikao na wahusika kueleza jinsi walivyosimamia na kutekeleza miradi ya maji wilayani humo.  Aweso alisema hayo katika kikao hicho alichotaka asitumwe mwakilishi bali wahusika wenyewe.
usudi la Naibu Waziri Aweso  ilikuwa kushiriki kikao hicho ili kubaini changamoto zote za miradi ya maji wilayani Karatu na kutafuta jibu ili maji safi na salama yawafikie wananchi na wadau wengine kwa wakati kama serikali ilivyopanga.
Mapema Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mahongo, alimwambia Aweso kwamba, miongoni mwa changamoto za miradi ya maji wilayani hamo ni mapungufu ya kiusanifu. Ambapo alidai hali hiyo ilitokana na miradi ilipoanza kutekelezwa 2012/2013 haikufanyiwa mapitio ya usanifu upya, baada ya Mtaalam Mshauri Kampuni ya Tanplanet Njegimi Express kuachishwa kazi kwa kutokidhi viwango.

No comments:

Post a Comment

Pages