Na Talib Ussi, Zanzibar
Serikali ya Mapinduzi
ya Zanzibar (SMZ) imepiga marufuku ndege zote zinazoleta wageni (Watalii) kutoka nje
kuingia Zanzibar na wale ambao wataingia kwa kutumia chata za ndani wawekwe
karantin kwa kutumia gharama zao wenyewe kwa muda wa siku 14.
Akizungumza na
waandishi wa habari Kaimu wa Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo, katika ziara maalum ya kutembelea vituo
vilivyotengwa kwa ajili ya kuwatibu wagonjwa waliopata maambukizi ya virusi vya
Corona huko Kidimni Wilaya ya kati Unguja alifahamisha kuwa kwa sasa Zanzibar ina
mgonjwa mmoja na hawataki kuongeza wengine.
Alisema wamezuiya
safari zoote za watalii kuja Zanzibar ili kupambana na maradhi hayo katika
visiwa vya Zanzibar hadi pale
itakapotolewa taarifa nyengine.
“Na yeyote atakayekuja
atalazimika kukaa ndani kwa siku 14 kwa gharama zake na hili ni tamko rasimini
la SMZ” alieleza Mahmoud.
Alieleza kuwa mamlaka
husika zoote usafirishaji watalii ikiwemo uwanja wa ndege, Uhamiaji na yale mashirika binafsi tayari
wameshawaeleza hilo.
“Kwa sababu dunia mzima
imechukua hatua hiyo tayari imechukua hatua hii nadhani wageni watakuwa
wachache sanaa” alisema.
Alisema hivi sasa
mahotel karibuni 95% tayari zimefungwa na zilizobakia ni chache mnoo ,a ambazo
zinawageni kutoka Urusi na idadi yake ni 506 na kueleza kuwa nahao pia
wataondoka kwa ndege yao maalum inayokuja kutoka nchini kwao na kuondoka nao
jumamosi (leo).
“Sisi hatuwezi kuwafukuza
raia wa kigeni kiholela hasa nchi ambazo tunafanya nazo kazi vizuri lakini kwa
wakati huu kila mmoja anajua jangaa lililoikumba dunia”
Alieleza kwa upande wa
makampuni yametoa mashikirikiano mazuri sanaa na ya kiungwana na na kuleleza kuwa wako tayari
kwa chochote kile kwa maslahi ya taifa.
Pia aliwaomba wageni
ambao wana nia ya kuja visiwani Zanzibar kwa kipindi hichi wasubiri kwanza
mpaka pale haya maradhi yatakapodhibitiwa , alisema kuwa yoyote ambaye ataingia
nchini awe tayari kuka chibi wa uwangalizi kwa siku 14 kwa gharama zake
mwenyewe.
Kwa upande wake
mkurugenzi Kinga Dk. Fadhil Muhammed
aliwataka wananchi kusikiliza maelekezo ya kiafya ili kuepuka ugonjwa huo.
Awala Zanzibar ilifungiya
mashirika ya ndege ya Italy kuingia Visiwani Zanzibar kwa ajili ya kuzuia
ugonjwa huo kuingia nchini.
Alisema hadi sasa Zanzibar
ina mgonjwa mmoja tu ambaye ni raiya wa Ghana aliyotokea Ujarumani.
No comments:
Post a Comment