Tukiadhimisha
‘Siku ya Wanawake Duniani’, Benki ya
NMB imekua katika mstari wa mbele kuunga
mkono kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani #EachForEqual, ambayo inaangazia Usawa kwa Wote.
Katika
Maadhimisho yaliyofanyika kitaifa Wilayani
Bariadi Mkoani Simiyu mapema leo, NMB imekua miongoni mwa wadhamini wakuu walionogesha
maadhimisho hayo kwa kutoa shilingi Milioni 26 ambapo pesa taslimu ni milioni 5
pamoja na fulana zenye thamani ya shilingi Milioni 21.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan (kulia),
akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa NMB -
Vicky Bishubo, alipotembelea banda la benki hiyo mjini Bariadi Mkoani Simiyu
kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani. Kulia kwake ni Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto - Ummy Mwalimu.
Kaimu
Mkurugenzi wa Benki ya NMB - Ruth Zaipuna, akizungumza kwenye maadhimisho ya
siku ya Wanawake Duniani, yaliyofanyika kitaifa Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu- Antony Mtaka (Kushoto) akifurahia
jambo na Mbunge wa Urambo - Margaret Sitta, Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya NMB
-Ruth Zaipuna na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi- Sospeter Magesse.
Wakiongozwa na
Kaimu Mkuruzenzi wa Benki ya NMB-Ruth Zaipuna kwa pamoja wanasema ‘Usawa kwa Wote’
Tunawatakia,
kheri ya Siku ya Mwanamke!
#NMBBankKaribuYako
No comments:
Post a Comment