Baadhi ya wahamiaji haramu 51 ambao ni raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa kwa
kos ala kuingia nchini bila ya kibali wakiwa wamekamatwa wakiwa wamejificha
katika kichaka ambacho kipo karibu na pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya
hindi(Picha na Victor Masangu).
Baadhi ya wahamiaji haramu 51 ambao ni raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa kwa
kos ala kuingia nchini bila ya kibali wakiwa wamekamatwa wakiwa wamejificha
katika kichaka ambacho kipo karibu na pembezoni mwa ufukwe wa bahari ya
hindi.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Bi. Zainabu Kawawa akiwa ananawa mikono baada ya
kutoka kuwaangalia wahamiaji haramu wapatao 51 ambao wamekamatwa kwa kuingia
nchini bila ya kuwa na kibali maalumu katika maeneo ya kichaka kimoja kilichopo
ufukweni mwa bahari.
Baadhi ya wahamiaji haramu raia wa Ethiopia ambao wamekamatwa kutokana na
kuingia nchini bila ya kuwa na kibali
wakiwa katika moja ya kituo cha afya kwa ajili ya kuangaliwa afya zao ikiwemo
kuwapima kama wanamaambukizi ya magonjwa mbali mbali ikiwemo ugonjwa wa
Corona.
Na Victor Masangu, Bagamoyo
JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani
limewakamata Wahamiaji haramu 51 walioingia nchini kupitia bandari bubu ya ya
Makurunge Tarafa ya Yombo Wilayani Bagamoyo Mkoani hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Pwani Wankyo Nyigesa alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, ambapo alisema
wahamiaji hao walikamatwa majira ya saa 11 alfajiri Mach 19.
Wankyo alisema, watuhumiwa hao
walikabidhiwa kwa vyombo vingine vya dola kwa taratibu za kisheria waweze
kuchukuliwa hatua.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na
usalama wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa alisema, wahamiaji hao wamekutwa
katika pori wakiwa katika harakati za kutafuta usafiri kuelekea Mikoa ya Nyanda
za juu Kusini ili waweze kuendelea na safari yao hadi Afrika Kusini.
Kawawa lisema, Wahamiaji hao
walikuwa wanaotokea nchini Ethiopia, ambao katika mahojiano ya awali walikiri
kuingia Nchini kwa kupitia Pwani ya Bagamoyo, wakitumia majahazi.
Alisema, Wahamiaji hao walichukuliwa
hadi katika kituo cha Afya Matimbwa (Bagamoyo) ili kupimwa kama Wana maambukizi
ya Virusi vya Corona.
Kituo hicho kilichotengwa na
Halmashauri kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wa Corona wanaoweza kujitokeza siku
za usoni, .
Wahamiaji hao, wamefikishwa katika
kituo hicho ili kufanyiwa vipimo vya awali kujiridhisha kama hawana maambukizi
ya ugonjwa wa Corona, kabla ya kupelekwa katika gereza la Kigongoni
Wilayani Bagamoyo wakisubiri kusomewa mashtaka yao ya kuingia Nchini bila
kibali
Wakati huo huo, Jeshi la Polisi
Mkoani Pwani linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji na
kufukia mwili wa marehemu..
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani
Wankyo Nyigesa alisema, watuhumiwa hao walikamatwa Machi 19 huko Kibindu Wilaya
ya Bagamoyo wakituhumiwa kuua na kuzika mwili wa marehemu (jina
linahifadhiwa)katika shamba la mahindi.
Wankyo alisema, Machi 3, majira ya
saa nane mchana huko Kibindu mtuhumiwa Chacha Machangu (27) alimfumania mke
wake akiwa na mwanaume mwingine .
Kamanda alisema, Machangu
alimshambulia mke wake kwa kumkata na panga maeneo mbalimbali ya mwili wake na
kumsababishia majeraha yaliyopelekea kifo.
Wankyo alisema, Machangu kwa
kushirikiana na ndugu zake Emmanuel Machangu (19) na Hamis Machangu (22
walichimba shimo kwenye shamba la mahindi na kufukia mwili wa marehemu.
Kamanda alibainisha kuwa, Machi 19
Jeshi la Polisi lilipata taarifa kutoka kwa wasamaria wema ambapo lilifanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao watatu ambao walionyesha shimo lilipo na
lilipofukuliwa mwili wa marehemu ulipatikana.
Alisema, mwili wa marehemu
ulifanyiwa uchunguzi na daktari na kufanyiwa mazishi kwa kufuata taratibu.
Jeshi hilo limesema, bado
linaendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaodaiwa kushiriki katika tukio hilo.
No comments:
Post a Comment