Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent
Bashungwa, akitolea ufafanuzi wa bei ya barakoa ambapo ameagiza bei isizidi 1500
badala
ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500 ambayo watanzania wengi inawapa
changamoto ya kumudu. (Picha na Eliud
Rwechungura, Wizara ya Viwanda na Biashara).
Waziri wa Viwanda na Bishara, Innocent Bashungwa (kulia) akipokea
maelezo kutoka kwa Emmanuel Mgoma (kushoto)
muakilishi wa kiwanda cha Sunflug ambacho kwa sasa kinazalisha barakoa 25,000
kwa siku. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
Waziri wa Viwanda na Bishara Mhe Innocent Bashungwa akizungumza na
menejimenti ya kiwanda cha A to Z ambacho kwa sasa kinazalisha barakoa 15,000 kwa siku.
Arusha, Tanzania
Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, amesema atachukua hatua kwa Taasisi zisizo za kiserikali
(NGOs) zinazouza barakoa kwa gharama kubwa.
Bashungwa alitoa taadhari
hiyo mkoani Arusha alipotembelea Viwanda vya kuzalisha nguo vya Sunflug na A to
Z kuangalia hali ya uzalishaji wa barakoa katika Viwanda hivyo.
Bashungwa alitoa onyo kwa
NGOs zilizoomba kibali cha kuzalisha barakoa kwa ajili ya kuwasaidia Watanzania
lakini badala yake wanauza barakoa kwa shillingi 2,500 hadi 3,000
“wamekuwa wakitoa masharti
kupitia mitandao ya kijamii kuwa hawauzi barakoa chini ya bei hiyo”.
Sitawataja kwa leo lakini
nikiona tu wanauza kwa bei kubwa sitasita kuwachukulia hatua, maana mnakuja
kuomba vibali kumbe mnafanya mtaji.
Aliongeza kusisitiza barakoa
zote ziuzwe kwa bei isiyozidi 1500 badala ya bei ya sasa ilikuwa sokoni ya 2500
ambayo watanzania wengi inawapa changamoto ya kumudu.
Aidha Bashungwa alivipongeza Viwanda nguo vya A-Z na Sunflug kwa kuzalisha barakoa
ambazo zinawasaidia watanzania walio wengi, na amewahaidi serikali kuwapati ushirikiano.
Aidha alivitaka Viwanda hivyo
kuendelea kuzalisha kwa wingi ili wananchi walio wengi wa vijijini waweze
kupata vifaa hivyo vya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa korona.
Kwa upande wake mkuu wa Mkoa
wa Arusha, Mrisho Gambo, aliwataka wananchi wote wa mkoa huo kuchukua
taadhali zinazotolewa na Wizara ya afya wanapotembelea maeneo yenye mkusanyiko.
Pia, alisisitiza kuwa ni vema
sasa wafanyabiashara hao wakatengeneza barakoa kwa bei nafuu ili kuwezesha
wananchi kununua.
Wakitoa taarifa kwa
Waziri, Emmanuel Mgoma mwakilishi wa kiwanda cha Sunflug alisema kiwanda
kina uwezo wa kuzalisha barakoa 25,000 kwa siku.
Mwakilishi wa A-Z,
Slyvester Kazi, alisema kiwanda kina
uwezo wa kuzalisha barakoa 15,000 kwa siku.
No comments:
Post a Comment