April 30, 2020

Benki ya CRDB yaichangia Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete Sh. Milioni 50 kwa ajili ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya JAKAYA KIKWETE Prof . Mohamed Janabi amesema watu wenye matatizo ya kiafya ya Moyo, kisukari, saratani, matatizo ya kifua kama vile pumu, figo na wale wenye umri mkubwa wanatakiwa kuchukua taadhari kubwa zaidi dhidi ya COVID - 19, kwani makundi hayo ndio waathirika wakubwa ya VIRUSI vya CORONA.

Prof Janabi ameyasema hayo leo Aprili 30, 2020, jijini Dar es Salaam wakati wa kupokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh million hamsini kutoka benki ya CRDB, ikiwa ni ukamilishaji wa ahadi iliyotolewa na benki hiyo ya million mia moja, kwaajili ya kusaidia upasuaji kwa wagonjwa kwenye taasisis hiyo ya moyo hasas watoto, ambapo mwaka jana tayari walishatoa million hamsini za awali.

Prof Janabi amesema fedha hizo ambazo benki ya CRDB iliahidi kutoa mwishoni mwa mwaka wa fedha 2020 lakini wamezitoa sasa zimekuja wakati muafaka, kwani changamoto za COVID - 19,  moja ya makundi ambayo ni waathirika wakubwa ni wale wanye magonjwa ya moyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mawasiliano wa benki ya CRDB Tully Ester Mwambapa amesema, benki yake imeamua kutoa sasa kwasababu wanaamini COVID - 19 imeleta changamoto nyingi ambazo zinatakiwa kutatuliwa kwa wakati.

Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akizungumza wakati alipofika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo, ikiwa ni kukamilisha ahadi yake ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 100. Kulia ni Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi, akizungumza wakati wa hafla fupi ya kupokea mchango wa  shilingi milioni 50 uliotolewa na Benki ya CRDB kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Esther Mwambapa (kushoto) akimkabidhi  Mkurugenzi  Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Prof. Mohamed Janabi mfano wa hundi ya shilingi milioni 50 kwa ajili ya upasuaji wa moyo kwa watoto wanaotibiwa katika Taasisi hiyo, ikiwa ni kukamilisha ahadi yake ya kuchangia kiasi cha shilingi milioni 100 ili ziweze kufanikisha upasuaji wa moyo kwa  watoto, makabidhaino hayo yamefanyika leo jijini Dar es salaa.

No comments:

Post a Comment

Pages