Na Tiganya Vincent
HALMASHAURI ya
Wilaya ya Kaliua katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Machi imenunua bandali
300 kwa gharama ya milioni 80 kutokana na mapato ya ndani.
Kauli hiyo imetolewa
jana na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Haruna Kasele wakati wa kikao cha Baraza
la Madiwani.
Alisema bati hizo
zitagawanywa katika Kata zote ambazo zimekamilisha mabona, ununuzi wa mbao na
vifaa kwa ajili ya upauaji.
Aidha , Mwenyekiti
huyo aliongeza kuwa wanaendelea na ujenzi wa vyumba 6 vya maabara katika shule
za sekondari ya Kanoge, Kamsekwa, Zugimulole, Silambo, Seleli na Ilege.
Katika hatua
nyingine Kasele alisema Kaliua imeshapokea shilingi bilioni 1 kwa ajili ya
mpango wa elimu bila malipo kutoka Serikali
kuu.
Alisema kwa upande
wa shule za Msingi wamepokea shilingi milioni 683.9 na shule ya sekondari
wamepokea shilingi milioni 399.8.
Kasele aliishukuru
Serikali kwa kutoa fedha hizo ambazo zimewawezesha wanafunzi kujiunga na Shule
za Msingi na Sekondari katika uongozi wa awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Wakati huo huo
Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua imetoa jumla ya mikopo ya shilingi milioni 345
kwa vikundi mbalimbali.
Kasele alisema shilingi
milioni 133.5 zimetolewa kwa vijana, shilingi milioni 184 zimetolewa kwa wanawake
na milioni 27.5 zimetolewa kwa walemavu.
Alivitaka vikundi
ambavyo vimekopeshwa kuhakikisha wanarejesha fedha hizo ili ziweze kukopeshwa
kwa vikundi vingine.
No comments:
Post a Comment