Kaimu Meya wa Manispaa ya Iringa Joseph Nzala Ryata akiwa katika mtaa wa Kihodombi manispaa ya Iringa akizindua mkakati wa kukarabati wa barabara za manispaa ya Iringa mara baada ya mvua kupungua
Katapila likiwa katika mtaa wa Kihodombi likisembua Barabara ya mtaa huo ikiwa ni siku ya uzinduzi wa mkakati wa Halmashauri ya manispaa ya Iringa.
Na Fredy Mgunda, Iringa
Kaimu
Meya wa Manispaa ya Iringa, Joseph Ryata, amezindua rasmi mkakati maalum wa
Halmashauri ya Manispaa ya Iringa wa Ukarabati wa barabara za kata 18
zilizoharibika kutokana na mvua zzilizonyesha katika msimu wa masika.
Wakati
wa Uzinduzi wa Mkakati huo wenye lengo la kuondosha changamoto ya baadhi ya
maeneo kutofikika kirahisi na kukwamisha maendeleo ya wananchi wa manispaa ya
Iringa.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi huo kaimu meya alisema kuwa halmashauri imekuja na mkakati
wa kuhakikisha wanakarabati barabara zote zilizoharibiwa na mvua ya msimu huu
na kurahisisha shughuli za wananchi kuendelea kama ilivyokuwa hapo awali.
Alisema
mvua za msimu huu zimeharibu barabara pamoja na kuvunja madaraja madogo na
makubwa na kusababisha kukatika kwa mawasiliano katika baadhi ya mitaa ya kata
za manispaa hiyo na kusababisha shughuli za kiuchumi kuzorota.
Ryata alisema sababu ya kuanza kukarabati
barabara ya mtaa wa Kihondombi ni kutokana na umuhimu wa barabara hiyo ambayo
hutumika kama mbadala wa barabara kuu iendayo Hifadhi ya Taifa ya Ruaha iliyopo
mkoani Iringa.
“Ikitokea
ajali yoyote itakayolazimisha kufungwa kwa barabara kuu iendayo Hifadhi ya
Taifa ya Ruaha na endapo barabara ya Kihodombi haipitiki ni wazi kuwa ni ngumu
kwa watalii na watu mbalimbali kufika katika maeneo wanayotakiwa kufika kwa
mjibu wa watuaji wa barabara hiyo,hivyo ni sasabu mkuu ya kuanza ukarabati wa
barabara hii kwa maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla” alisema Ryata
Aidha
Ryata alisema kuwa amekuwa akipokea malalamiko mengi juu ya ubovu wa barabara
ambazo zilikuwa zinasababisha usumbufu wa usafiri katika meneo mengi ya mitaa
ya manispaa ya Iringa ambazo zilikuwa zinasababisha kushuka kwa uchumi wa
wananchi.
Kwa
upande wa baadhi ya wananchi wa maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Iringa
wamepongeza mpango huo wa Manispaa wakieleza kwa muda sasa shughuli mbalimbali
za kiuchumi zimekuwa zikikabiliana na changamoto kuu ya miundombinu duni ya
barabara kutokana na vyombo vya usafiri kushindwa kufika kwa wakati katika
maeneo husika huku wakilazikia kutumia gharama kubwa zaidi.
Nao
viongozi wa Serikali za mitaa ya kata ya Kihodombi Manispaa ya Iringa wameeleza
kuwa hatua hiyo inayosimamiwa na Kaimu Meya wa Manispaa ya Iringa ni ya
kipeekee kwani hakuna mwananchi anayechangishwa fedha ili kukarabati barabara
hizo zilizosahalika kwa muda mrefu na kusababisha wananchi kuichukia Serikali
yao
No comments:
Post a Comment