Katibu
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Joseph Nyamhanga (kushoto),
akimsikiliza Muhandisi wa Halmashauri ya Shinyanga Bw. William Lusiu kuhusu
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo jana alipofanya ziara ya Siku moja Mkoani
Shinyanga kujionea miradi ya maendeleo inayoendelea Mkoani Shinyanga, katikati
ni Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovera.
Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Eng. Joseph Nyamhanga
akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
ya Shinyanga jana alipofanya ziara ya
Siku moja Mkoani Shinyanga kujionea miradi ya maendeleo inayoendelea Mkoani
Shinyanga.
Katibu
Mkuu TAMISEMI Eng.Joseph Nyamuhanga pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Yasinta
Mboneko alipotembelea mradi wa machinjio ya kisasa yaliyoko nje kidogo ya mji
wa Shinyanga.
Katibu Mkuu TAMISEMI Eng. Joseph Nyamhanga akiwa na viongozi mbalimbali wa Mkoa
wa Shinyanga alipotembelea mradi wa machinjio ya kisasa yaliyoko nje kidogo ya
mji wa Shinyanga.
Na
Mwandishi Wetu, Shinyanga
Miradi mikubwa
inayoendelea katika Mkoa wa Shinyanga imetakiwa kwa kukamilishwa kwa wakati
ndani ya muda uliopangwa ili Serikali ianze kutekeleza miradi ya mwaka mpya wa fedha
kama iliyopangwa kufanyika katika bajeti mwaka wa fedha 2020/21.
Agizo hilo kwa
Serikali ya Mkoa wa Shinyanga lilitolewa na Katibu Mkuu Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa Eng. Joseph Nyamhanga alipofanya ziara ya Siku moja Mkoani
Shinyanga kujionea miradi ya maendeleo inayoendelea Mkoani Shinyanga.
Miradi iliyotembelewa
na kiongozi huyo ni miradi mitatu iliyoko Manispaa ya Shinyanga inayojumuisha
Km 13.1 za barabara za Manispaa bil.15, Mradi wa Machinjio ya Kisasa ya nyama
wenye thamani ya sh. Bil.5 na ujenzi wa dampo la taka lenye thamani ya Sh.
Mil.400 miradi ambayo inatakiwa kukamilika ifikapo Juni 30, 2020.
Akiongelea kuhusu
ujenzi wa Machinjio ya Kisasa unaoendelea Mkoani Shinyanga Eng. Nyamhanga
alishauri uongozi wa Mkoa kuhakikisha unamsimamia mkandarasi wa mradi huo ili
aweze kukamilisha ujenzi wa mradi huo
kwa kipindi cha mwezi mmoja na
kuharakisha ufungaji wa majokofu ya kuifadhi nyama na miundombinu nyingine inayohusu
machinjio hayo ya kisasa.
Naye Mkurugenzi wa
Manispaa ya Shinyanga Bw.Geofrey Mwangulumbi aliyataja Machinjio hayo ya Kisasa
kuwa yana uwezo wa kuhifadhi ngo’mbe 100 kwa siku pamoja na kutoa huduma ya
nyama kwa wafanyabiashara mkoani Shinyanga na maeneo mengine nje ya mkoa huo.
Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga Bw. Albert Msovera aliongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutaongeza
udhibiti wa ubora wa nyama itakayokuwa inauzwa Mkoani hapo ikiwemo kuongeza
mapato ya Halmashauri pamoja na Serikali.
Pamoja na kutembelea
miradi hiyo ya Manispaa ya Shinyanga Eng. Nyamhanga pia alipata fursa ya
kutembelea ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya ya Shinyanga Vijijini iliyoko
Makao Makuu ya Wilaya hiyo yaliyoko Kata ya Iselamagazi Shinyanga vijijini
ambayo ni sehemu ya hospitali nyingine 98 zinazojengwa hapa nchini ambayo
ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 80.
Katibu Mkuu Nyamhanga
alionesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali hiyo yenye thamani ya sh.
mil. 500 na kupongeza uongozi wa Mkoa kwa kuweza kutumia kiwango hicho cha
fedha kuongeza jengo la kuifadhia maiti pamoja na jengo la mionzi kwani ujenzi
wa majengo hayo awali haukuwa sehemu ya makadilio ya fedha za ujenzi wa
hospitali hiyo.
Aidha Katibu Tawala
wa Mkoa wa Shinyanga Bw. Albert Msovela alimwambia kiongozi huyo kuwa Serikali
Mkoani Shinyanga itaendelea na usimamizi wa ujenzi wa wa hospital hiyo na
kutaja changamoto upungufu wa watumishi
wa Afya katika Wilaya hiyo na kuongeza kuwa mahitaji ya watumishi katika Wilaya
hiyo ni takribani watumishi 500.
Pamoja na changamoto
ya watumishi wa Afya Bw. Msovela aliongeza kuwa kukamilika kwa hospitali hiyo
kutasaidia kupunguza hadha za wakazi wa Iselamagazi na maeneo jilani kwani
awali walilazimika kutembea km 50 kufuata huduma za matibabu Shinyanga mjini.
Miradi hiyo mikubwa
inayoendelea Mkoani Shinyanga iko katika hatua za mwisho za utekelezaji wake
ikijumuisha miradi mingine iliyoko katika Wilaya nyingine Mkoani Shinyanga
amabayo pia inatarajia kukamilika kabla
ya kuanza kwa mwaka mpya wa fedha 2020/21.
No comments:
Post a Comment