Rais John Magufuli. |
Na Mwandishi Wetu
Rais John Magufuli amefanya
uteuzi mwingine mpya kwa kumteua Brigedia Jenerali Dk. Gabriel Mhidize kuwa
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD).
Taarifa ya Ikulu iliyosainiwa leo na
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Chato, Gerson Msigwa ilisema, uteuzi
wa Brigedia Jenerali Dk. Mhidize umeanza Mei 3, mwaka huu.
Taarifa hiyo ilisema kabla ya
uteuzi huo, Brigedia Jenerali Dk.
Mhidize alikuwa Mkuu wa Hospitali ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo Jijini Dar es Salaam.
“Brigedia Jenerali Dk. Mhidize
anachukua nafasi ya Laurean Bwanakunu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Hata hivyo taarifa hiyo ya
Ikulu haikueleza wazi sababu za kutenguliwa kwa Bwanakunu katika nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment