Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Zainab Telack, akikagua vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa Corona vilivyotolewa na Shirika la World Vision huku Mkurugenzi wa Shirika hilo Kanda ya Ziwa, John Massenza akiangalia.
Na
Mwandishi Wetu, Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa
Shinyanga Bi. Zainab Telack amepokea msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa
wa Corona wenye thamani ya Shilingi Milioni 29 kutoka shirika la World Vision
Kanda ya Ziwa kwa ajili ya watumishi wa Afya walioko mstari wa mbele kupambana
na ugonjwa huo katika mkoa wa Shinyanga.
Akiongea mara baada
ya makabidhiano ya vifaa hivyo Bi. Zainab Telack amesema kuwa vifaa hivyo ni
msaada mkubwa kwa waudumu wa afya kwani vitawasaidia wafanyakazi hao kuwaudumia
wagonjwa wa corona kwa amani kwa kuwa watakuwa na uhakika wamejikinga ipasavyo.
Mkuu huyo wa Mkoa
aliongeza kuwa baadhi ya vifaa vilivyotolewa na Shirika hilo vitawezesha pia
watendaji kutoa elimu kwa wananchi wakiwa mbali bila kulazimika kuwa katika
msongamano kwani shirika hilo limechangia pia vipaza sauti kwa ajili ya kutoa
elimu maeneo ya vijijini.
Bi. Zainab Telack
amewataka waudumu wa afya pamoja na wananchi kwa ujumla wasichoke na kuendelea
kujikinga na kuwakinga wengine kwa kuwa ugonjwa wa corona hauchagui lakini pia
haujulikani uko kwa nani nakuwataka wadau, wananchi pamoja na serikali
kushiriki katika mapambano dhidi ya corona.
Akiongea na waudumu
wa Afya mara baada ya kukamilisha kazi ya kupokea vifaa hivyo Bi. Zainabu
Telack aliwataka waudumu hao kufikiria kutumia njia mbadala ikiwemo matumizi ya
mitishamba iliyopendekezwa na wataalam
wa Afya ikiwemo kujifukiza kwa kuwa ugonjwa huu mpaka sasa hauna tiba
maalum iliyopendekezwa.
‘’Baadhi ya watu
wametumia dawa za kujifukiza na kupata nafuu kubwa na ninyi tumieni dawa hizi kupambana
na ugonjwa huu kwani kila mmoja wetu akifanya jitihada za kutokomeza ugonjwa
huu tunaweza kuumaliza’.’ Alisisitiza Mkuu huyo wa Mkoa.
Mkurugenzi wa Shirika
la Word Vision Kanda ya Ziwa Bw. John Massenza amevitaja vifaa vilivyotolewa na
shirika lake kuwa ni Gloves, Magauni ya Kujikinga, Vitakasa Mikono, Vipasa
sauti pamoja na barakoa na kuongeza kuwa tayari Shirika lake limetoa mafunzo
kwa watoa huduma ngazi ya jamii, vituo vya Afya na baadhi ya madiwani Wilayani Shinyanga.
Aidha Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile ameshukuru uongozi wa Shirika hilo kanda
ya Ziwa na kuwataka wadau wengine kuendelea kushirikiana na serikali kuchangia
vifaa vya kujikinga na Corona na kuwezesha watoa huduma ya Afya kujikinga na
kuwadumia wagonjwa kwa usalama na uhakika.
Serikali Mkoani Shinyanga
inaendelea kuelimisha jamii ikiwemo kuhakikisha watu wanavaa barakoa pamoja na
kuepuka misongamano katika minada ya mifugo ikiwemo kupiga maarufuku wazazi
kwenda na watoto katika maeneo yenye mikusanyiko.
No comments:
Post a Comment