May 08, 2020

UWANJA WA KUMBUKUMBU YA SOKOINE MBEYA WAANZA KUANDALIWA KWA MICHEZO YA LIGI KUU

Muonekano wa Uwanja wa Sokoine.


 
Na Kenneth Ngelesi, Mbeya

BAADA ya Rais Dk. John Magufuli kusema anafikiria kuruhusu kuendelea kwa shughuli za michezo nchini, wamiliki wa uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya wameanza  kusafisha uwanja huo ikiwa ni maandalizi ya kutumika kwa michezo ya ligi kuu Tanzania bara na igi daraja la kwanza.

Baada ya serikali kuzuia shughuli za michezo kwa lengo la kuepusha msongamano ikiwa ni tahadhari ya maambukizi ya virusi vya corona, viwanja vingi vya michezo nchini vilitelekezwa bila matunzo.

Meneja wa Uwanja Kumbukumbu ya Sokoine Modesutus Mwaluka alisemam baada baada ya Rais Dk. John Magufuli kutamka kuwa anafikiria kurejesha shughuli za michezo, kauli hiyo imezindua na ndiyo maana wameanza kuufanyia marekebisho ikiwemo kufyeka nyasi na kuweka alama.

‘Kauli ya Rais Magufuli imetukumbusha kuwa tunapaswa kuwa tayari wakati wote na ndiyo maana tumeamua kuanza zoezi ya kufyeka nyasi na kuweka alama’ alisema Mwaluka.
  
Baadhi ya wadau wa michezo Jijini Mbeya Yohana Nazareth na Venance Siulanga waliipongeza hatua na Wamiliki wa Uwanja kuamua kufanya maandalizi na kutaka wasimamizi na wamiliki wa viwanja vingine vyote vya michezo nchini kuiga mfano huo.

‘Kiukweli sasa uamuzi ulifanywa na wamilikia wa Uwanja wa Sokoine ni wakuigwa na wasaimamizi na wamiliki wengine wa viwanja kuendelea kuvitengeneza mana huenda kauli ya Mh Rais Magufuli ikatekelezwa muda wowote” alisema  Siulang.

Uwanja wa kumbukumbu ya sokoine uliopo jijini mbeya, unatumiwa  kama uwanja wa nyumbali wa timu za ligi daraja la pili za Tukuyu stars,ligi daraja la kwanza Mbeya Kwanza,na Boma Fc na timu za ligu kuu ni Mbeya city na Tanzania Prisons.

No comments:

Post a Comment

Pages