Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela akishiriki
uzinduzi wa Mradi mpya wa taasisi ya Save The Children ambapo mradi huo mpya
utajikita katika kuongeza ushiriki wa wananchi katika michakato ya kisera na
Kibajeti.
Na Mwandishi Wetu
Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. Nicodemus Mwangela amewataka wadau kwa kushirikiana na
serikali waendelee kutoa msaada kwa watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi
kwani bado wengi hawajafikiwa.
Brig. Jen. Mwangela
ameyasema hayo wakati akishiriki uzinduzi wa Mradi mpya wa taasisi ya Save The
Children ambapo mradi huo mpya utajikita katika kuongeza ushiriki wa wananchi
katika michakato ya kisera na Kibajeti.
Amesema taasisi hiyo
imekuwa ikisaidia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi hivyo miradi
mingine watakayo ianzisha wasisahau lengo kuu la taasisi hilo la kusaidia
watoto kwakuwa bado wapo wengi wenye matatizo ambao bado hawajafikiwa.
Brig. Jen. Mwangela
amesema wadau hao wa Save the Children pamoja na wengine wanaendelea kualikwa
kuwasaidia watoto walioko katika mazingira hatarishi pia kutoa elimu kwa jamii
kwakuwa bado elimu ya kupambana na ukatili wa watoto bado haijafika kote.
Ameongeza kuwa mradi
huo mpya ulioanzishwa ni mzuri na tayari serikali imesha fanya kwa hatua kubwa
hasa kwa kuboresha huduma za kijamii kama elimu, maji na afya pamoja na kutoa
uwazi kwa wananchi kushiriki katika huduma hizo hivyo wadau wanapaswa
kusaidiana na serikali katika jitihada ambazo tayari zimeanzishwa.
Meneja Mradi wa
kuongeza ushiriki wa wananchi katika michakato ya kisera na kibajeti kwa Mkoa
wa Songwe John Tobongo amesema mradi huo unatarajia kufanyika katika Wilaya ya
Mbozi Mkoa wa Songwe, Shinyanga na Zanzibar na utagharimu Euro laki tano.
Tobongo amesema
matarajio ya mradi huo ni kuwafikia wananchi wa Mbozi 524,450 huku ukijumuisha
na watoto pia utatekelezwa kwa mwaka 2020 hadi 2021.
No comments:
Post a Comment