July 11, 2020

BALOZI WA UJERUMANI AMSIFU JPM KUKUZA UCHUMI

 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Benny Mwaipaja, (wa tatu kushoto) akiwaongoza wawakilishi wa Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo kumkaribisha Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, alipofika kujionea huduma na elimu inayotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, akisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa Tehama wa Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Emmanuel Maendaenda, kuhusu Mfumo wa Malipo ya Serikali kwa njia ya Kielektroniki (GePG) wenye lengo la kuongeza uwazi na udhibiti wa fedha za umma, kuboresha na kurahisisha namna ya kulipia huduma za umma, katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika uwanja wa maonesho wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 Afisa Masoko na Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa UTT AMIS Bw. Rahim Mwanga akimweleza Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, namna mifuko ya uwekezaji wa pamoja inavyowasaidia wananchi wa vipato vya chini kushiriki katika uwekezaji wa masoko ya fedha na mitaji, wakati balozi huyo alipofika kujionea huduma na elimu inayotolewa na Wizara pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utafiti, Ushauri na Machapisho wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA), Dkt. Abdallah Gorah, akitoa maelezo kwa Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Regine Hess, kuhusu mafunzo yanayotolewa na chuo hicho kwa wajasiriamali wadogo yenye lengo la kuwawezesha kuwa na nidhamu ya fedha pamoja na kuweza kusimamia vizuri mikopo mbalimbali wanayopata ili kuweza kujikwamua kiuchumi, wakati Balozi huyo alipotembelea banda la Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Taasisi zake katika Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam.
 (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha na Mipango)

No comments:

Post a Comment

Pages