July 10, 2020

BENKI YA STANDARS CHARTERED TANZANIA YATOA MSAADA WA SH. BILIONI 1.2 KWA UNICEF NA RED CROSS


 
Na Janeth Jovin


BENKI  ya Standard Chartered Tanzania imetoa msaada wa Sh. Bilioni 1.2 ambazo ni sawa na dola za kimarekani 550,000 kwa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania (Red Cross) na kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF). 

Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam ilieleza kuwa kati ya fedha hizo, Sh. Milioni 690 ambazo ni sawa na dola za kimarekani 300,000 zimekabithiwa kwa Red Cross Tanzania kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa dhana za kujikinga ikiwepo maji safi na salama na sabuni. 

Ilieleza kiwa kiasi cha Sh.Milioni  575 sawa na dola za kimarekani 250,000, zimekabidhiwa kwa UNICEF kwa ajili ya kuendelea kutoa elimu hususan kwa watoto waishio katika mazingira yenye changamoto.  

"Misaada hii ni sehemu ya ahadi ya Standard Chartered PLC ya dola milioni10 ambapo milioni tano kwa msalaba Mwekundu na dola milioni 1.5 kwa UNICEF ambazo zitawasaidia katika shughuli za dharura hasa wakati huu wa mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 huko Asia na Afrika," ilieleza taarifa 

Aidha ilieleza kuwa Sanjay Rughani ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo ya Standard Chartered Tanzania, alisema "Standard Chartered Tanzania inajivunia kuweza kuchangia juhudi mbalimbali za Msalaba Mwekundu na UNICEF zinazowafikia watu walio hatarini zaidi katika jamii zetu. Kwa kufanya kazi na mashirika haya, tunaweza kusaidia juhudi zinazoendelea ambazo zinalenga kushughulikia baadhi ya changamoto muhimu zilizotokana na janga la COVID-19, "

Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Msalaba Mwekundu Tanzania, Julius  Kejo amesema anaishukuru kwa msaada huo kwani utakwenda kunisaidia jamii zinazokumbana na changamoto mbalimbali kutokana na janga la virusi vya corona.

"fedha hizi zitasaidia kushughulikia baadhi ya athari za haraka za kiafya na kijamii zinazowakabili watu walio hatarini zaidi katika nchi yetu. Shukrani kwa mchango muhimu kutoka kwa Standard Chartered, sasa tunaweza kuendelea kusaidia watu zaidi wanaokabiliwa na athari mbaya za virusi vya corona. "

Mkurugenzi, Idara ya Fedha ya Kibinafsi ya UNICEF na Ushirikiano, Gary Stahl  amesema "Tunashukuru kwa mchango huu kutoka Standard Chartered, UNICEF itaweza kusaidia elimu ya mbali kupitia runinga, redio, simu za mkononi na kufanya ulinzi  kwa watoto walio katika mazingira hatarishi ulimwenguni."

No comments:

Post a Comment

Pages