July 19, 2020

Gwajima; sijawahi kubadilika


Na Asha Mwakyonde
 
NDUGU wa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na uzima, Josephat Gwajima, Wakili  Msomi wa kujitegemea Methusela Gwajima amesema yeye ni Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambaye hajawahi kubadilika.

Gwajima ni miongoni mwa watia nia  176 waliochukua fomu za kuomba ridhaa ya kuteuliwa na chama hicho   Jimbo la Kawe  Oktoba 25.

Akizungumza leo jijini  Dar es Salaam amesema kuwa lengo la kuchukua fomu hiyo ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli katika kipinchi ya miaka mitano ya uongozi wake.

Wakili huyo amesema suala la makada wa CCM kujitokeza kwa wingi kuwania jimbo la Kawe kunaonyesha kuna demokrasia ya kweli katika chama hicho.

Gwajima amesema kuwa chama hicho kimeweka utaratibu mzuri wa uchukuaji fomu na  urejeshaji kwamba yeye ni kada wa CCM ambaye hajawahi kubadilika.

'Mimi ni kada wa chama cha mapinduzi na sijawahi kubadilika hivyo nimeona kuna kila sababu ya kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuwania nafasi ya  ubunge katika jimbo la Kawe,'amema Gwajima.

amesema kuwa kati ya watia nia 176 mmoja akayepata nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Kawe 175 watamuunga mkono.

No comments:

Post a Comment

Pages