July 11, 2020

MKUTANO MKUU WA CCM JIJINI DODOMA LEO

 MWENYEKITI wa CCM Taifa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia matokeo ya Uchaguzi ya Mgombea Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupeperusha bendera ya CCMm wakati wa Mkutano Mkuu  wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma(Picha na Ikulu).
 WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa CCM wakishangilia wakati wa hafla hiyo ya ufunguzi wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu)
 MGOMBEA Urais wa Zanzibar kwa Tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Mhe.Dkt. Hussein Ali Hassan Mwinyi akizungumza na Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu)
 MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu)
 MSANII wa Kizazi kipya Bongo Flava Diamond  akitoa burudani kwa Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi wakati wa mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma.(Picha na Ikulu)

No comments:

Post a Comment

Pages