July 17, 2020

MWANAMKE WA 50 KUCHUKUA FOMU KILIMANJARO NI HINDU LUGOME

Na Dixon Busagaga, Moshi

KUNDI la vijana ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) mwaka huu ni wazi limehasika baada ya kujitokeza kwa wingi kuchukua fomu kwa lengo la kuwania nafasi ya kupewa ridhaa ndani ya chama hicho ya kupeperusha Bendera katika ngazi za majimbo.

Jina la Hindu Lugome si geni katika siasa za Jimbo la Vunjo ambapo katka uchaguzi wa mwaka 2015 ni miongoni mwa waliotia nia akiwa na umri mdogo wakati huo miaka 25 na sasa amerejea tena akiwa na umri wa miaka 30 akijaribu kutafuta nafasi hiyo kwa mara nyingine.
Bi Hindu Lugome akikabidhiwa fomu za kuwania ubunge katika jimbo la Vunjo ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) akiwa miongoni mwa kundi la Wanawake 50 waliojitokeza kuwania ubunge kupitia majimbo ya mkoa wa Kilimanjaro.
Bi Hindu Lugome akikamilisha zoezi la ulipiaji wa ada kwa ajili ya fomu ya kuwania Ubunge ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Vunjo.
Bi Hindu akionesha fomu yake aliyochukua kwa ajili ya kuwania Ubunge katika jimbo la Vunjo ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

No comments:

Post a Comment

Pages