July 09, 2020

MWENYEKITI WA CCM RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA USALAMA NA MAADILI YA CHAMA CHA MAPINDUZI CCM PAMOJA NA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM KATIKA UKUMBI WA JAKAYA KIKWETE JIJINI DODOMA

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa amesimama pamoja na Wajumbe wa Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama cha Mapinduzi CCM kumkumbuka aliyewahi kuwa Waziri katika Baraza la kwanza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere Marehemu Balozi Job Lusinde aliyefariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili ya Chama cha Mapinduzi CCM kilichofanyika leo tarehe 09 Julai 2020 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini
Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein kabla ya kuanza kwa kikao cha Kamati Kuu kilichofanyika leo tarehe 09 Julai
2020 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiimba Wimbo wa Chama pamoja na Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM kabla kuanza kwa Kikao hicho cha Kamati Kuu kilichofanyika leo tarehe 09 Julai 2020 katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM jijiji Dodoma.
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Rais
Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Katibu Mkuu wa CCM Dkt. Bashiru Ally Kakurwa wakati akitoka katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma mara baada ya kuongoza vikao vya Kamati ya Usalama na Maadili pamoja na Kamati Kuu leo tarehe 09 Julai 2020. PICHA NA IKULU.

No comments:

Post a Comment

Pages