July 20, 2020

NMB YAZIPIGA TAFU SHULE 6, KITUO CHA AFYA KINONDONI

 
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo, akipokea msaada mabati 180 kutoka kwa Kaimu Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam - Seka Urio.  
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Turiani wakipeleka madawati darasani baada ya hafla fupi ya makabidhiano na Benki ya NMB. 


Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB, imekabidhi misaada ya mabati 180, madawati 200, mashine sita za kunawia mikono, viti na meza 100, kwa ajili ya Shule za Msingi Oysterbay, Msasani, Tandale Magharibi, Mzimuni na Kisauke pamoja na Sekondari ya Turiani. Huku kituo cha Afya cha Mabwepande kikipata vitanda magodoro, vyote kwa pamoja vikiwa na thamani ya jumla ya Sh. Mil. 36.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya kuvibabidhi kwa Mkuu wa Wilaya - Daniel Chongolo, Kaimu Meneja wa Benk ya NMB Kanda ya Dar es Salaam - Seka Urio alisema “Ingawa Serikali inafanya makubwa, sisi kama wadau tunawajibu wa kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo kwa kusaidia jamii, kwani kupitia jamii hii hii, ndio imeifanya benki yetu kuwa hapa ilipo, kubwa kuliko benki yoyote hapa nchini huku tukiendelea kupokea tuzo ya benki bora kwa mara ya nane mfululizo,”
 
Alibainisha kuwa, NMB itaendelea kushirikiana na Serikali katika kuleta maendeleo katika jamii inayowanzunguka. “Kwa maana hiyo, NMB tumeamua kushirikiana na shule hizo,  ambazo kila shule inapata madawati 50 na viti vyake. Pia tumechangia Shule ya Msingi Mzimuni mabati 150, huku Shule tano zikipata mashine za kunawia mikono na maji tiririka ilikuzuia maambukizi ya Covid-19,” aliongeza:
 
Kwa mwaka 2020, NMB imetenga zaidi ya Sh. Bilioni 1 kwa ajili ya kuchangia maendeleo ya jamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya na elimu, kiasi kinachoifanya kuwa benki ya kwanza katika kuchangia maendeleo kuliko benki yoyote nchini.
 
Kwa upande wake, DC Chongolo aliipongeza Benki ya NMB kwa moyo wa kuijali na kuithamini jamii na kwamba misaada mbalimbali inayotoa katika sekta za afya na elimu, inaacha alama njema katika mioyo ya wanafunzi, walimu na jamii kwa ujumla na kuwa inasaidia harakati za Serikali katika kuboresha miundombinu na kutatua changamoto.
 
Chongolo aliwaagiza watendaji mbalimbali waliopo katika Wilaya ya Kinondoni, kuhakikisha wanatumia huduma za NMB hasa za makusanyo ya kodi, ili kuchagiza pato la benki hiyo na kukuza asilimia moja ya mapato yao yamwaka na kuzifikia taasisi nyingi zaidi zenye uhitaji kupitia program ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR).

No comments:

Post a Comment

Pages