July 09, 2020

Siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu yawakutanisha Wabunifu katika Maonesho ya Sabasaba 2020

NA TATU MOHAMED

SERIKALI imesema kuwa uzalishaji viwandani unategemea kwa kiasi kikubwa matumizi ya teknolojia mpya na ubunifu, hivyo ni muhimu kuzalisha wataalamu wengi nchini.

Hayo yalibainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dk. Leonard Akwilapo, alipozungumza na waandishi wa habari katika mjadala wa Siku ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu ambao uliowakutanisha wabunifu, watafiti wa Sekta Binafsi, uliofanyika katika viwanja vya Maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba'.

Dk. Akwilapo amesema uzalishaji wa wataalaamu wa teknolojia wakitoka nje ya nchi itakua ghali na inawezekana isiendane na mazingira yake kuliko teknolojia hiyo ikizalishwa nchini.

"Viwanda vikiimarika vikichukua mazao kwa wakulima, wakulima watapata faida, Wafanyabiashara pamoja na Viwanda na pato la taifa litaongezeka zaidi"alisema

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia-(COSTECH) Dk. Amosi Nungu amesema kuwa kwasasa nchi imeingia kwenye uchumi wa kati hivyo ili iweze kufikia juu inahitajika nguvu ya pamoja.

Kwa upande wake Mbunifu wa Tuzo za Costech kwa mwaka 2011, 2015 na 2019 George Buchafwe amesema kuwa wamebuni  mashine za kuchakata mchikiti na kutengeneza sabuni, kutokana na serikali kutangaza zao hilo kuwa miongoni mwa mazao ya kimkakati.

Ameongeza kuwa, wamejikita zaidi kuliongezea thamani zao hilo kwa kutengeneza sabuni, mafuta na chakula.

No comments:

Post a Comment

Pages