July 15, 2020

Ubalozi wa Uholanzi waipatia THRDC kiasi cha Sh. Milioni 60

Na Janeth Jovin

MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeushukuru Ubalozi wa Uholanzi hapa nchini kwa kuwasaidia kiasi cha Sh. Milioni 60 kwa ajili ya kutumika katika kuboresha shughuli mbalimbali za utetezi wa haki za binadamu.

Akizungumza leo wakati wa kusaini mkataba wa kupokea fedha hizo, Mratibu wa Kitaifa wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema fedha hizo pia zitatumika katika kujenga ushawishi na mahusiano kati ya Watetezi wa haki za binadamu na taasisi mbalimbali za Serikali.

Amesema mkataba wa fedha hizo ambao utakaodumu kwa Kipindi cha mwaka mmoja kuanzia Julai 2020 hadi Julai 2021, unalenga pia kutoa  msaada wa kisheria kwa Watetezi wa haki za binadamu nchini, huku wanufaika wakubwa wa mradi huo wakiwa ni watetezi wa haki za binadamu.

"Tunawaomba watanzania wafahamu kuwa tumeweza kusaini mkataba huu wa fedha hizo na imekuwa utaratibu wetu kuwatangazia kila fedha za misaada tunazopatiwa kutoka kwa wahisani," amesema

No comments:

Post a Comment

Pages