Wakazi
wa Wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro wameatakiwa kuanza kufikiria namna
bora ya kuleta maendeleo katika jimbo hilo badala ya kutumia muda mwingi
katika migogoro na kuridhika na vitu vidogo wanavyopewa na wanasiasa
baada ya kuwachagua.
Hayo
yamesemwa na mtia nia wa ubunge katika jimbo la Kilosa aliyeibuka
kidedea katika kura za maoni Prof. Palamagamba John Kabudi alipokuwa
akitoa shukrani zake mara baada ya kuchaguliwa na wana ccm wenzake
katika kinyang’anyiro cha kura za maoni kupitia chama cha mapinduzi
jimbo la Kilosa.
Kabla
ya kutangaza matokeo hayo yaliyoendeshwa kwa njia ya uwazi msimamizi wa
uchaguzi huo Bw Mohamed Mzee amesema yeye hana mamlaka ya kumtangaza
mshindi bali anamtangaza aliyeongoza kwa kupata kura nyingi huku
akiwaasa vijana kuwa wavumilivu na wenye nidhamu wanapoamua kuingia
katika siasa.
Uchaguzi
wa kura za maoni kupitia Chama cha Mapinduzi katika jimbo la Kilosa
ulikuwa na watia nia 29,ambapo kura 1013 zilipigwa na wajumbe
waliohudhuria ambapo kura tano ziliharibika ambapo katika kura hizo
aliyeongoza ni Prof. Palamagamba John Kabudi aliyejizolea kura
714,Mshindi wa pili Bw. Kaunda Alfat Saidi amepata kura 101 na mshindi
wa tatu amepata kura 51.
No comments:
Post a Comment