July 21, 2020

WALIOSHINDA KURA ZA MAONI CCM HAWA HAPA

NA JANETH JOVIN

Prof. Kitila aongoza kura za maoni Ubungo

Aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Profesa Kitila Mkumbo ameshinda kura za maoni za kugombea Ubunge jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam.

Katika kura hizo za maoni zilizofanyia leo Prof. Kitila amependekezwa kwa kura 172 kati ya kura 375 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa jimbo hilo. Wagombea katika kinyang;anyiro hicho walikuwa 110.

Prof. Kitila amewashinda watia nia 109 akiwamo aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii Shamsa Mwangunga aliyepata kura tisa na Katibu wa MsaidiziIdara ya Siasa, Uhusiano wa Kimataifa CCM Bara Mwantum Mgonja aliyepata kura 73.

Kabla ya kuingia katika Chama cha Mapinduzi, Profesa Kitila alikuwa mshauri wa Chama cha ACT- Wazalendo na alijiondoa katika chama hicho mara baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji.

Ndugulile ambwaga Makonda kura za maoni Kigamboni



Aliyekuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Faustne Ndugulile ameshinda kura za mani za kugombea ubunge jimbo la Kigamboni.

Ndugulile ameshinda kwa kupata kura 190 huku mpinzani wake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ambaye amepata kura 122.

Mchakato wa upingaji kura katika jimbo hilo ulikuwa na ushindani mkali hasa kutokana na wagombea kukubalika na wajumbe wa mkutano wa kuchagua wawakilishi
 

Zungu aongoza kura za maoni jimbo la Ilala
 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu ameongoza kura za maoni katika katika Jimbo la Ilala baada ya kupata kura 148 akifuatiwa na aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo, Sophia Mjema aliyepata kura 103.

No comments:

Post a Comment

Pages