August 07, 2020

BENKI YA CRDB YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA TAASISI YA REPOA

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano na Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Maendeleo ya Jamii (REPOA) ambapo katika ushirikiano huo taasisi hiyo itaiongezea benki hiyo uwezo mkubwa wa kufanyakazi zake pamoja na uwekezaji, utoaji huduma za kifedha katika sekta zote za uzalishaji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Sera na Uchumi (REPOA), Dk. Donald Mmari, akizungumza wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa ushirikiano na Benki ya CRDB.

Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts (kushoto), akisaini mkataba wa ushirikiano na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Sera na Uchumi (REPOA), Dk. Donald Mmari.
Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambo, akisaini mkataba huku Mkuu wa Kitengo cha Mikakati Benki ya CRDB, Jessica Nyachiro, akishuhudia.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti, Sera na Uchumi (REPOA), Dk. Donald Mmari, wabadilishana mikataba waliyosaini.
Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya CRDB, Dk. Joseph Witts (kulia) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti Sera na Uchumi (REPOA), Dk. Donald Mmari, wakionesha mikataba waliyosaini.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Pages