August 13, 2020

Benki ya NMB Yanogesha Siku ya Kizimkazi Zanzibar

Benki ya NMB inaendelea kuboresha miundombinu na mazingira ya shule visiwani Zanzibar kwa kutoa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi Milioni 10/- zilizofanikisha ujenzi wa vyoo vyenye matundu 10 katika shule ya Kibuteni iliyopo Wilaya ya Kusini. NMB pia imetoa tisheti 300- ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono sherehe za Kizimkazi ‘Kizimkazi Day’ zinazofanyika kila mwaka mwezi wa nane - Lengo ikiwa ni kutathmini shughuli za kimaendeleo katika maeneo ya Kizimkazi na kuangali changamoto zilizopo ili kuzipatia utatuzi.
Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Maafisa wa Benki ya NMB katika hafla ya kukabidhi msaada wa vyoo vya matundu 10 vyenye thamani ya sh. Milioni 10/- kwa shule ya Msingi Kibuteni iliyopo Zanzibar Wilaya ya Kusini.


Siku hii huratibiwa na Makamu wa Rais- Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na viongozi wengine wa Serikali visiwani humo. Akizungumza katika hafla ya makabidhiano, Mheshimiwa Samia ameishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyokuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii mbalimbali kama Elimu, Afya na Maafa. 

Ni miaka mingi sasa, Benki ya NMB imekua ikitoa asilimia 1℅ ya faida yake kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii
inayowanzunguka.

Makamu wa Rais Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi kutoka kwa Meneja wa NMB kanda ya Dar es Salaam- Donatus Richard alipotembelea akina mama wajasiriamali wanaodhaminiwa na Benki hiyo kwenye hafla ya Kizimkazi Day Wilaya ya Zanzibar. Akishuhudia ni Meneja Masuala ya Uwajibikaji kwa Jamii – Bi Lilian Kisamba (mwenye koti).

 

Akizungumza Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam - Donatus Richard ameeleza kuwa, utoaji wa elimu kwa vijana ni suala la kipaumbele sana na kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu NMB imekuwa ikiwawezesha vijana kupata elimu ya fedha na kujifunza kuweka akiba katika umri mdogo kupitia program yake ya WAJIBU -Jifunze, Jipange Wajibika’ – katika shule za msingi na secondary Tanzania. ikilenga vijana kujifunza umuhimu wa kuweka akiba na mipango kwaajili ya maendeleo yao na kukidhi mahitaji muhimu ya baadae. 

Kupitia program hii wameweza kuwafika zaidi ya vijana 70,000 nchini.

Jengo la choo cha matundu 10 lililokabidhiwa na Benki ya NMB kwa matumizi ya wanafunzi wa shule ya Msingi Kibuteni Zanzibar Wilaya ya Kusini. 


NMB inatambua kwamba ili mtu aweze kuimarika kifedha, ni lazima ajenge mtazamo unaofaa kuhusu matumizi ya fedha. Hivyo basi, wamekuwa wakiwaelimisha Wajasiriamali Wadogo na wa Kati; Kupitia Klabu za Biashara za NMB, wajasiriamali wa kati na wadogo wamekuwa wakipewa elimu juu ya masuala yanayohusu mipangilio ya biashara, utunzaji wa vitabu vya fedha, mipangilio ya fedha, kukopa na elimu katika maeneo mengine ya fedha kama yalivyoombwa na wanachama. 

No comments:

Post a Comment

Pages