August 11, 2020

BILIONI 10 ZATENGWA KWA AJILI YA TAASISI ZA UTAFITI WA MAZAO

 

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Jerard Kusaya, akiangalia baadhi ya mazao katika Kituo cha Utafiti Maruku.

 

 

Na Lydia Lugakila, Kagera


Kiasi cha shilingi bilioni 10 zimetengwa na serikali nchini kwa mwaka huu wa fedha wa 2020-21 kwa ajili ya kuziwezesha taasisi za utafiti wa mazao kutekeleza shughuli zake kwa ufanisi.
 
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Jerard Kusaya, wakati alipotembelea kituo cha utafiti Maruku na kwamba taasisi hizo zinao mchango mkubwa katika kuhakikisha sekta ya kilimo nchini inakua kwa kuongeza uzalishaji hasa katika mazao ya kimkakati yanayokuwa yamepangwa na serikali kwa kuzalisha mbegu bora.

Amesema kuwa ili tija iweze kupatikana kupatikana ni lazima taasisi hizo ziwezeshwe na kwamba mbali na fedha shilingi bilioni 10 iliyotengwa kwa mwaka huu katika mwaka wa fedha uliopita serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 3 na kwamba matunda yamekuwa makubwa nchini yatokanayo na utafiti wa mazao na elimu inayotolewa na taasisi hizo.

Kwa upande wake mkuu wa kituo cha utafiti Maruku Dr,John Sariha amesema kuwa licha ya kituo hicho kukabiliawa na changamoto ya watumishi bado hali ya uzalishaji itokanayo na matumizi ya mbegu bora zinazozalishwa na kituo hicho mkoani Kagera unaongezeka kwa kiasi kikubwa.

No comments:

Post a Comment

Pages