Lissu amesema kauli hiyo ni ‘Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watanzania’.
Lissu
ameyaeleza hayo jana akiwa Jimbo la Kawe ikiwa ni muendelezo wa chama
hicho kuzindua kampeni katika jiji la Dar es Salaam lwa siku tatu
mfululixo.
Lissu akowa jimboni hapo amesema, chochote kilichopo kwenye ilani ya chama chao kinabeba msingi wa kauli mbiu hizo..
Amesema
ilani yao ya Uchaguzi Mkuu huu ina kauli mbiu yenye maneno yafuatayo
ambayo ni Uhuru, Haki na Maendeleo ya Watu’, na kuongeza kuwa chochote
ambacho wamekisema katika ilani hiyo msingi wake ni uhuru wa watu na
maendeleo ya watu.
“Maendeleo tunayoyataka ni yanayozingatia
uhuru wa watu, yanayozingatia haki zao, maendeleo aliyoyaita Baba wa
Taifa maendeleo ya watu badala ya vitu” amesema Lissu.
August 31, 2020
Chadema yatangaza kauli mbiu yake Uchaguzi Mkuu 'Uhuru, haki na Maendeleo ya Watu'
Mgombe
wa Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),
Tundu Lissu, ameweka wazi kuwa kauli mbiu itakoyobeba ilani ya chama
chao.
Mgombea Urais Tundu Lissu na Mgombea Mwenza Salum Mwalimu wakionesha Ilani ya Chadema kwa Uchaguzi Mkuu wa 2020 baada ya kukabidhiwa rasmi na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Freeman Mbowe katika uzinduzi uliofanyika jana Uwanja wa Tanganyika Parkers, Kawe, jijini Dar es Salaam. (Picha na Chadema).
Wananchi wakifuatilia mkutano wa uzinduzi wa kampeni za Mgombea Urais wa Chadema, Tundu Lissu katika Uwanja wa Liwiti, Segerea jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment