August 23, 2020

KOKA ATINGA OFISI ZA MKURUGENZI NA TREKTA KUCHUKUA FOMU ZA UBUNGE JIMBO LA KIBAHA MJI

Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha Mji, Silvestry Koka, akiwapungia mkono wananchi na wanachama wa CCM kutoka sehemu mbalimbali waliojitokeza kwa ajili ya kumsindikiza kwenda kuchukua fomu katika ofisi za Mkurugenzi wa Uchaguzi zilizopo Kibaha Mji. Kushoto kwake ni mke wake Mama Selena Koka.
 Mbunge mteule wa kuwania nafasi ya ubunge katika Jimbo la Kibaha Mji, Silvestry Koka (kulia), akipokea fomu za ubunge  kutoka kwa mkurugenzi wa uchaguzi jimbo la Kibaha mjini Jenipher Omolo kulia katika ofisi zake ambako alifika ofisini hapo akiwa na mkewe wakiwa wamepanda gari aia ya Treka.

 

         

VICTOR MASANGU, PWANI

 

              Viongozi a chama cha mapinduzi ambao alishindwa katika mchakato wa kura za maoni wametakiwa kuachana na makundi na badala yake wahakikishe kwa sasa wanaungana kwa pamoja na kuwaunga wagombea wote waliopitishwa kuwania katika nafasi mbali mbali ili kuweza kuleta ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu ambao unatarajiwa kufanyika octoba 28 mwaka huu.

 

             Kauli hiyo imetolewa na   Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Elias Mpanda  wakati wa halfa ya kuwatambulisha wagombea waliopitishwa katika kura za maoni katika nafasi za udiwani pamoja na nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Kibaha mjini.

               Katibu huyo alibainisha kwamba kwa sasa mchakato wa zoezi la kura za maoni zimeshamalizika kwa hivyo wanachama wote wa CCM pamona na wale wagombea wote ambao walishiriki katika kugombea nafasi mabali mbali wanatakiwa kuwa kitu kimoja kwa kushirikiana bega kwa bega katika harakati za kampeni na kuachana na chuki.

             “Kwa mimi nilishakuwa katibu wa chama katika mikoa mbali mbali na mkoa wa Pwani ni Mkoa wa Tano hivi, hivyo kitu kikubwa ninachowaomba ndugu wanachama wote wa CCM, kipindi hiki tulichonacho ni kipindi cha kuelekea katika uchaguzi mkuu kwa hivyo tunatakiwa tushikamane vya kutoshe,”alisema Katibu huyo.

              Pia  katibu huyo aliwahimiza wagombea wote ambao wamepata fusra ya kupitishw majina yao wahakikishe kwamba wanatekeleza ilani ya mapinduzi kwa kuhakikisha kwamba wanasikiliza kero za wananchi na kuwaletea maendeleo katika Nyanja mbali mbali ikiwemo sekta ya elimu maoja pamoja na mambo mengine.

             Kwa upande wake Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka alisema lengo lake kubwa ni kuendele akushirikiaa bega kwa began a wananchi wa jimbo hilo sambamba na kuhakikisha kwamba anamalizia ahadi zake ambazo aliziahidi katika kipindi cha nyuma pamoja na kuwaletea maendeleo wananchi.

              Pia Koka aliongeza kuwa anamshururu Rais wa awamu ya tano Dk John Pombe Magufuli kw akuwezakuleta miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta mbali mbali ikiwemo ujenzi wa zahanati mbali mbali, vituo vya afya pamoja na hospitali za wilaya aambazo zimeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kuwasaidia wananchi katika upatikananji wa huduma ya afya.

             “Mimi napenda kuwashukuru wanacham wote wa CCM na viongozi wa CCM, ngazi mbali mbali kwa kuniteuwa kupeperusha bendera tena ya kuwa Mbunge mteule wa Jimbo la Kibaha mjini na mimi nina imani kwa kushirikiana na serikali pamoja na viongozi wangu wa chama tutaendelea kuwatumikia wananchi katika suala zima la kutatua changamoto zao zinazowakabili,”alisema Koka. 

              Kadhalika Mbunge huyo mteule wa jimbo la kibaha mjini alisema kwamba kwa sasa kwa upande wake ataungana na wenzake wote ambao walikosa nafasi katika mchakato mzima wa kura za maoni na kwamba amewaomba kuwa kitu kimoja na kuachana na makundi na badala yake wachape kwazi kwa umoja ili kuweza kuleta maendeleo chanya katika jimbo la Kibaha mji.

              Koka ambaye leo amekwenda kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo ya Ubunge jimbo la Kibaha mjini amepolelea na umati wa wanachama wa CCM kutoka kata mbali mbali 14 za Jimbo hilo pamoja na viongozi mbali mbali kwa ajili ya kwenda kuchukua fomu katika ofisi z amkurugenzi wa uchaguzi uku akiwa amepanda katika gari aina ya Treka.

No comments:

Post a Comment

Pages