August 08, 2020

Mahakama yahairisha kesi ya kupinga ubaguzi kwenye uchaguzi

Na Janeth Jovin

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya  Dar es Salaam imeahirisha kesi ya kupinga ubaguzi kwenye uchaguzi iliyofunguliwa na Mratibu wa Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu Onesmo Olengurumwa.

Mahakama ilitarajiwa kutoa uamuzi wa mapingamizi ya awali yaliyotolewa na wajibu maombi leo, Tarehe 6 Agosti 2020 lakini imeshindwa kufanya hivyo kwani uamuzi huo haujakamilika na hivyo kupelekea kuahirishwa kwa kesi hiyo.

Olengurumwa alifungua kesi hiyo September 16, 2019 akiishtaki Wizara ya ofisi ya Rais, Utawala wa Mkoa na Serikali za mitaa pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Tanzania.

Historia fupi iliyosababisha kufunguliwa kwa shauri hilo

Kwa kuzingatia matakwa ya kikatiba kuhusu namna ya kuendesha nchi kidemokrasia, mlalamikiwa ambaye ni Waziri wa Tamisemi, kwa mamlaka aliyonayo kisheria alitangaza kuitisha uchaguzi wa serikali za mtaa nchini Oktoba 24, 2019.

Katika kutekeleza majukumu hayo alitunga na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali, Kanuni za kusimamia uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019.

Kanuni hizo zilitangazwa kwenye: Tangazo la Serikali Namba 371 la Mwaka 2019  na Tangazo la Serikali Namba 373 la Mwaka 2019 zilizotungwa kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) sura ya 287 (Toleo la Mwaka 2002); pamoja na Tangazo la Serikali Namba 372 la Mwaka 2019 na Tangazo la Serikali Namba 374 la Mwaka 2019 zilizotungwa kwa Mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Mji) sura ya 288 (Toleo la Mwaka 2002).

Ndani ya Kanuni hizo, vifungu mbalimbali vilitungwa ili kutoa sifa za raia wa Tanzania kugombea na kuchaguliwa. Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la Serikali Namba 371 la Mwaka 2019 na Kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali 373 la Mwaka 2019 zilizotungwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) sura ya 287 (Toleo la Mwaka 2002) na

Kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali Namba 372 la Mwaka 2019 na Kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali Namba 374 la Mwaka 2019 zilizotungwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Mji) sura ya 288 (Toleo la Mwaka 2002) zinazuia watu wenye umri kati ya miaka 18 hadi 21 kugombea na kuchaguliwa kwenye nafasi za uongozi.

Dhumuni la Olengurumwa kufungua kesi hiyo ni kuwa watanzania  wenye umri kati ya 18 na 21 wanazuiliwa kisheria kuwania nafasi kwenye uchaguzi bila sababu za msingi za kisheria.

Mapingamizi ya awali yaliyotolewa na Mwanasheria Mkuu

Katika shauri hilo, Mwanasheria Mkuu alitoa mapingamizi yafuatayo kwanza Ubaguzi wa kiumri ni wa halali na wa busara ukiwa na dhumuni la kumtafuta mtu sahihi kushika nafasi hiyo ya kisiasa na kuwa umelenga katika kusawazisha wajibu wa atakayechaguliwa kushika nafasi hiyo ya kisiasa.

Pili Mwanasheria Mkuu wa Serikali amesema katika mapingamizi yake kuwa Serikali ina Haki ya kuweka sababu za msingi ili kupunguza kiwango cha kufurahia Haki na  uhuru.

Pia Kwamba kizuizi cha miaka Katika uchaguzi kimetokana na historia ya uchaguzi.

Hata hivyo Olengurumwa alifungua kesi hiyo ili kuomba amri zifuatazo kutolewa kwanza,  Kwamba kulingana na Ibara ya 12(2), 13(2), 21(1) na 29(1)  za Katiba ya Tanzania ( Sura ya 2 Toleo la 2002), watanzania wenye umri kati ya 18 na 21 wana Haki ya kuhusika na mambo yanayohusu Umma ambayo yanahusisha Haki ya kuwania nafasi Katika uchaguzi, Haki ya kupata huduma za umma ikiwa bi pamoja na kushiriki kama wagombea katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa Tarehe 24.11.2019.

Pili zuio la miaka Katika kuwania nafasi kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Tarehe 24.11.2019 kama lilivyowekwa chini ya kifungu cha 39(2)(b) cha Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa (Sura ya 292 Toleo la 2002) na chini ya Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la serikali la 371 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 372 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 373 la 2019 na     Kanuni  ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 374 la 2019  linakinzana na Ibara za 12(2), 13(2), 13(4), 21(1) na 29(1)  za  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Sura ya Pili Toleo la 2002) kwani halina sababu ya msingi na limelenga kuleta ubaguzi.

Tatu, kifungu cha 39(2)(b) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Sura ya 292 ya 2002) na Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la Serikali la 371 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 372 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 373 la 2019; na, kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 374 la 2019 ni kinyume na Katiba na zinapaswa kuondolewa kwenye vitabu vya Sheria za Jamhuri ya Tanzania.

Nne, Kwamba wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wenye umri kati ya 18 na 21 wana ruhusa na wataruhusiwa kuwania nafasi za kiserikali Katika uchaguzi Mkuu unaofuata.

Hata hivyo Olengurumwa amesema sababu kuu za kufunguliwa kesi hiyo, Kwamba katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, inapinga ubaguzi kwa misingi ya umri na  zuio hilo halijafuata taratibu za kuweka zuilio na hivyo ni kinyume na Katiba.

Pili,  kifungu cha 39(2)(b) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Sura ya 292 ya 2002) na Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la Serikali la 371 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 372 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 373 la 2019; na, kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 374 la 2019  zinakiuka Ibara za 12(2), 13(2), 13(4), 21(1) na 29(1) za Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ( Sura ya 2 Toleo la  2002) kwani vinaleta ubaguzi kwa msingi wa umri.

Tatu, kifungu cha 39(2)(b) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Sura ya 292 ya 2002) na Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la Serikali la 371 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 372 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 373 la 2019; na, kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 374 la 2019 vinakosa malengo yoyote na sababu za msingi za kutetea ubaguzi huo wa kiumri.

Nne, zuio lilipo chini ya kifungu cha 39(2)(b) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Sura ya 292 ya 2002) na Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la Serikali la 371 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 372 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 373 la 2019; na, kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 374 la 2019 halina umuhimu na halihitajiki kwani linawanyima Haki kinda kubwa la watu haswa wale wenye umri kati ya miaka 18 na 21.

5. Kwamba zuio la kiumri lilipo chini ya kifungu cha 39(2)(b) cha Sheria ya Serikali za Mtaa (Sura ya 292 ya 2002) na Kanuni ya 14(b) ya Tangazo la Serikali la 371 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 372 la 2019; kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 373 la 2019; na, kanuni ya 15(b) ya Tangazo la Serikali la 374 la 2019 halijazingatia hali za kijamii nchini ambapo watu wenye umri kati ya 18 na 21 wanachukuliwa kama watu wazima na wamekuwa wakihusishwa Katika kutoa maamuzi kwenye Jamii za Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages