August 02, 2020

MMILIKI WA SHULE ZA SEKONDARI ASHINDA UBUNGE VITI MAALUMU WAZAZI KILIMANJARO

Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha akiwa ameshikilia namba yake wakati akiomba kura kwa wajumbe wa mkutano mkuu wa Jumuiya ya wazazi mkoa wa Kilimanjaro. 
Wagombea wa nafasi ya Ubunge Viti Maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro wakiwa wameshikilia namba zao wakizonesha mbele ya Wajumbe (hawapo pichani) wakati wa kuomba kura ,kutoka kulia ni Zaina Heshima,Tusajigwe Ngwira ,Luisivivy Machange,Florance Sawe na Ester Rwegasha . 
Wajumbe kutoka wilaya ya Moshi vijijini wakipiga kura.


Wajumbe kutoka wilaya ya Same wakipiga kura. 
Msimamizi wa Uchaguzi ,Jonathan Mabiya akihesabu kura zilizopigwa huku Wagombea wakishuhdia zoezi hilo. 
Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi Ester Rwegasha akitia saini fomu za matokeo mara baada ya kuongoza katika kura za maoni . 
Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha (kushoto) akiwa na mshiriki aliyeshika nafasi ya pili baada ya kumshinda kwa kura moja pekee Tusajigwe Ngwira .  
Mshindi wa kura za maoni Ubunge viti maalumu kundi la Wazazi mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha (kushoto) akiwa na wagombea wengine mara baada ya kumalizika kwa zoezi la uchaguzi kwa jumuiya hiyo.


Na Dixon Busagaga, Kilimanjaro

 JUMUIYA ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi imefanya chaguzi za kura za maoni ikiwa ni mara ya kwanza kwa Jumuiya hiyo kupata uwakilishi wa Wabunge wa viti maalumu katika Bunge la Jamhuri ya muungani wa Tanzania ambapo kwa Kilimanjaro Mjane Ester Rwegasha ameshinda nafasi hiyo.

Nafasi ya Ubunge Vitimaalumu kupitia jumuiya ya Wazazi kwa mkoa wa Kilimanjaro imegombewa na makada Sita wa Chama cha Mapinduzi huku wajumbe 38 wa mkutano mkuu wa Jumiya ya Wazee mkoa wa Kilimanjaro wakifanya maamuzi ya kupata mwakilishi wa jumuiya hiyo.

Waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ambayo baadae atashindanishwa na washindi wengine kutoka mikoa 31 ya Tanzania bara ni pamoja na  Zaina Heshima ,Luisivivy Machange ,Flora Mbaga ,Florance Sawe ,Tusajigwe Ngwira na Ester Rwegasha.

Msimamizi wa Uchaguzi ,Jonathan Mabiya alimtangaza Ester  Rwegasha kuongoza katika zoezi la kura za maoni baada ya kupata kura 18 akimpita kwa kura moja mshindani wake Tusajigwe Ngwira aliyepata kura 17.

Katika kura za awali Ester Rwegasha na Tusajigwe Ngwira walifungana baada ya kila mmoja kupata kura 15 kati ya kura 38 zilizopigwa hali iliyomlazimu msimamizi wa Uchaguzi ,Mabiya kutangaza awamu nyingine ya upigaji kura kwa wawili hao.

“Walioudhuria ni 38 na kura zilizopigwa ni 38 ,hakuna kura iliyoharibika ,kura halali zikawa 38 ,Zaina Shabani Heshima amepata Sifuri,Luisivivy Machange amepata Sifuri, Flora Mbaga amepata kura 1, Florance Mushi amepata 7,na wafuatao kwa pamoja walifungana ,Tusajigwe Ngwira 15 na Ester Rwegasha 15.”alitangaza Mabiya.

Akizungumza mara baada ya kutangaza matokeo Jonathan Mabiya ambaye pia ni katibu wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Kilimanjaro alisema Kilimanjaro anapelekwa mtu atakaye kuwa mbunge kupitia jumuiya hiyo.

“Tutaenda Dodoma kwa wingi ili Kilimanjaro ipate mbunge wa kundi la Wazazi ,kule taifa wazazi wana nafasi mbili mbili, moja kutoka Zanzibar na  moja kutoka bara ,sasa hiyo moja tupeleke mtu ambaye watasema kweli Kilimanjaro imeleta mshindani na sio mshiriki.”alisema Mabiya .

Mshindi wa kura za maoni kupitia Jumuiya ya Wazee mkoa wa Kilimanjaro Ester Rwegasha aliyefiwa na mumewe miaka mitatu iliyopita kwa ugonjwa wa Saratani ya Tumbo alisema yapo mengi yamemgusa katika jumuiya ya Wazazi na kwamba huu ndio muda wa kuyatekeleza.

“Nimekuwepo katika Jumuiya yetu hii ya wazazi, nikiwa kama mwalimu yapo mambo ambayo nimeyaona yamegusa moyo wangu sana kiasi cha kuumia ,nina kili mbele yenu mimi ni mzalendo wa nchi yangu.na nina ipenda sana nchi yangu”alisema Rwegasha.

“Mbali na maujukumu ambayo ninayo ya kila siku nimedhamiria kutoka kwenye kilindi cha moyo wangu ,nimekuja kwenye Jumuiya yetu hii ya wazazi ,ili tuweze kushirikiana pamoja tuzifufue shule zote ambazo zimekufa,na zile ambazo hazifanyi vizuri”aliongeza Rwegasha

Suala la kubuni miradi ni miongoni mwa masuala ambayo Rwegasha amelipa kipaumbele huku akiweka mkakati kwa wilaya zisizokuwa na miradi kwa jumuiya ya Wazazi kupata miradi ili kuongeza kipato kwa jumuiya hiyo.

“Nina nguvu nina uwezo wa kukimbia huku na kule ,mimi ni jasiri an naomba mniamini mnitume popote na nitakwenda kuwawakilisha vyema.” Alisema Rwegasha.

No comments:

Post a Comment

Pages