August 14, 2020

MTAMBO WA UPAKUAJI MAFUTA KUGHARIMU BILIONI 47

 Na Asha Mwakyonde


MAMLAKA ya Bandari Tanzania TPA inatarajia kukamilisha mradi wa ujenzi wa mtambo wa mafuta utakaorahisisha upakuaji wa mafuta bandarini ambao umegharimu Tsh. bilioni 47.


 Haya yamesema jijini Dar es Salaam jana na Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe wakati wa ziara yake bandarini hapo amesema alipofika TPA alikuta changamoto mbili kubwa.


Amezitaja changamoto hizo kuwa  ni za fromita kutokupima kwa usahihi na kutokuwapo kwa matenki ya serikali ya kuhifadhia mafuta hayo. 


Waziri huyo amesema mitambo ya awali iliwasumbua ambapo Rais John Magufuli aliwaelekeza wanunue fromita mpya.
Mhandisi Kamwelwe ameeleza  kuwa mweshoni mwa mwezi Oktaba mitambo hiyo itakuwa imekamilika na kwamba watakuwa wameshasaini mitakatba ya ujenzi wa matenki ya kuhifadhiwa mafuta.


Amesema kuna bidhaa  kubwa za mafuta zinazopita badari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara  na kwamba awali walikuwa na mitambo ya kupitisha mafuta kutoka kwenye meli kwenda kwenye matanki ambayo iliwasumbua.


“Nilipoteuliwa kuwa waziri wa uchukuzi nilikuwa naangalia mahesabu ya lita ya mafuta iliyokuwa  ikiuzwa kwa mwananchi wa kawaida bei ilikuwa kubwa”,amesema Waziri Kamwelwe.


Waziri Kamwelwe amesema tayari tenda imeshatangazwa ya kujenga matenki hayo meli haitakuwa ikikaa siku tano tofauti na awali ilivyokuwa ikikaa  na kulipa fidia ya dola 20,000.


Ameongeza kuwa  kukamilika kwa matenki hayo mwananchi wa kwaida atapunguziwa gharama tofauti na awali walikuwa akiuziwa bei ya juu ya mafuta.


Alisema kuwa wanaendelea na ukaguzi wa mradi mkubwa wa ukarabati wa upanuzi wa bandari ya Dar es Salaam kwa ujenzi magati  nane ambayo moja la magari  na saba kwaajili ya makasha na mizigo ya nje.


Ameongeza kuwa wanapanua bandari ya Mtwara kwa kujenga gati moja kubwa la mita 300 na wanatarajia kusaini mkataba kwa ajili ya kujenga magati makubwa mawili katika bandari ya Tanga. 


amesema pamoja na ukarabati wa bandari kuna miundombinu ambayo ni ya lazima kurekebisha kutokana na maelekezo ya Rais Magufuli  aliwaelekeza wanunue skana za kutosha na tayari wamesha nunua.


Katika hatua nyingine Mhandisi Kamwelwe amezindua mifumo ya tehama ya ERP na e-ofisi ambao utarahisisha ufanyaji wa malipo kwa njia ya mtandao.


Naye Mkurugenzi Mkuu wa  TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoka amesema Rais Magufuli alifanya ziara Septemba 26 mwaka 2016 alitembelea eneo hilo ambapo alizungumzia mambo mawili ya Fromita na skana.


Amesema kwa Dar es Salaam kuna mita 19, Mtwara 4 ambazo ni dizeli na Petroli na kwamba Mtwara na Tanga  ni kwa ajili ya dizeli na Petroli   lakini tuna mita mbili za pamoja  ambazo ni kwa za mafuta ya ndege ya taa.


Amesema kwa hapa Dar es Salaam kuna kila aina ya mafuta yanayokuja ndio maana kuna mita 19 mafuta yanayopatika mbali na dizeli petroli, mafuta ya ndege,taa  na pia wataongeza mafuta ya kula, mazito,  mafuta ghafi ,vilainishi na  kutakuwa na mita kwa ajili ya gesi ya nishati.


“Faida zitakazopatikana ni pamoja na kuwa na upimaji wa uhakika zaidi, kuondoa udanganyifu unaofanywana wafanyabiashara kwa kushirikiana na wafanyakazi wachache kutoka taasisi za Umma”amesema.


Mhandisi Kakoko amesema mradi huo ulisainiwa Februari 28, mwaka jana na baada ya mwezi mmoja Machi 29, alikabidhiwa mkandarasi kuanza kazi ya kujenga mtambo huo.


Mkurugenzi huyo ameleza kuwa walikubaliana na Mkandarasi ifikapo mwishoni mwa mwezi Septemba mradi huo uwe umekamilika na Oktoba utaanza kufanyiwa majaribio na mafunzo kwa wafanyakazi watakao husika kutumia mtambo huo.
Amesema gharama zilizotumika kumlipa mkandarasi katika mradi huo nidola za kimarekani milioni 17.2 sawa na Tsh.bilioni 47 za kitanzania kwa mita zote 29.


Mhandisi Kakoko amesema kuhusu uendeshaji wa mradi huo wamekubaliana na taasisi 10 ambazo zitaleta wafanyakazi wao ili waweze kufanya kazi na TPA  na tayari  wameanza mfumo wa pamoja wauendeshaji.


Amesema kuwa wameshirikiana na Ofisi ya Rais kwa pamoja wanashughulikia eneo hilo kujenga na kwa uendeshiji wa mradi huo ambao utakuwa na wafanyakazi 111.


'Mheshimiwa Waziri utakumbuka hayo ndo maelekezo ya serikali yanatokana na hoja yako uliyoweka kwenye ngazi za juu za serikali kufanya ushirikiano,'amesema.


Ameongeza kuwa wafanyakazi hao 111  kwa ajili vituo vitatu ambapo Tanga 17, Mtwara 17 na Dar es Salaam 77 wote watakuwa chini ya Mkurugenzi Mkuu,Meneja kutoka TPA na watakuwa na maofisa mbalimbali kutoka katika taasisi hizo 10.

No comments:

Post a Comment

Pages