August 12, 2020

NDIKILO AANZA ZIARA BAGAMOYO

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza jambo na baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Pwani katika ziaara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamato zinazowkabili wananchi ambapo leo alikuwa katika wilaya Bagamoyo. (Picha na Victor Masangu).

 

 

VICTOR MASANGU, BAGAMOYO 

 

MKUU wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo amempongeza Rais wa awamu ya Tano Dk. John Pombe Magufuli kwa kupambana na kudhibiti na uingizaji wa madawa ya kulevya nchini na kuwataka vijana kuachana na tabia ya utumiaji wa madawa hayo yanapoteza kabisa  nguvu kazi ya Taifa.

Ndikilo ametoa kauli hiyo wakati wa  akizungumza na watumishi wa afya katika hospitali ya Bagamoyo, pamoja na baadhi ya vijana ambao wanapatiwa matibabu ya tiba za  madawa ya kulevya katika kliniki maalumu ya  Methodone iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani .

Alisema kwamba baadhi ya vijana wamekuwa wakipteza nguvu kazi kubwa ya Taifa kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya hivyo amewataka kuhakikisha kwamba wanabadilika na kujishughulisha kikamilifu katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo .

“Kwa kweli utumiaji wa madawa ya kulevya kwa vijana ni changamoto kubwa hivyo wanatakiwa kuachana kabisa na matumizi ya madawa ya kuelvya pamoja na uvutaji wa bangi, na pia ninawaomba wale wote ambao mpo katika kliniki hii kuzingatia elimu ambayo mnaipata na wataalamu wa afya ili kuepukana na madhara ya madawa hayo,”alisema Ndikilo.

Pia Ndikilo katika hatua nyingine ameutaka uongozi wa hospitali ya Bagamoyo kuhakikisha kwamba wanaweka nishati ya umeme katika jengo jipya ya kupumzikia watu mbali mbali ambao wanakwenda kuwaona  wagonjwa  ili waweze kupata fursa ya kuwa na mwanga nyakati za usiku.s

  Aidha Mkuu huyo akiwa katika ziara yake aliweza kutembeleaa katika shule ya sekondari ya Bagamoyo ambapo ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa hatua ambazo zimefanyika kwa kuweza kufanya ukarabati wa majengo mbali mbali kwa lengo la kuweza kuboresha sekta ya elimu kwa wanafunzi ili waweze kuongeza kiwango cha ufaulu.

Aliongeza kuwa serikali ya awamu ya tano imeweka kuweka mikakati madhubuti ya kukuza sekta ya elimu ili kuweza kukabilina na changamoto mbali mbali ambazo zilikuwepo hapo awali na kwamba lengo kubwa ni kuendelea kutoa elimu iliyo bora kwa wanafunzi pamoja na kufanya ukarabati wa majengo katika shule ambazo ni kongwe.

“Katika Mkoa wa Pwani tuna viwanda vingi kwa hii hili jambo lipo ndani ya uwezo wangu hivyo nitahakikisha kwamba tunalifanyia kazi kwa kushirikiana na wadau mbali mbali wa maendeleo ili kuweza kuhakikisha kwamba sekta ya elimu inafika mbali na kuweza kuwafanya wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.

Ndikilo Pia akiwa anazungumza na wananchi wa Wilaya ya Bagamoyo aliwataka wakulima na wafugaji katika maeeneo mbali mbali kuhakikisha kwamba wanaheshimiana bila ya kubaguana kwani serikai ya Mkoa wa Pwani wote inawajali na kuwathamini na kwamba itaendelea kushirikiana nao bega kwa bega katika shughuli mbali mbali za kimaendeleo.

No comments:

Post a Comment

Pages