August 17, 2020

RAIS WA ZANZIBAR DK. SHEIN AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA OFISI YA RAIS

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.  Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti  wa Baraza la Mapinduzi katika kikao cha  Utekelezaji Mpango Kazi kwa  kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 , kilichofanyika katika ukumbi wa  Ikulu Jijini Zanzibar, (kushoto kwa Rais) Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ndg.  Salum Maulid na (kulia kwa Rais) Katibu wa Baraza la Mapinduzi  na  Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee. (Picha na Ikulu)

BAADHI ya Watendaji wa Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza  la Mapinduzi, wakifuatilia ripoti ya Utekelezaji Mpango Kazi kwa kipindi  cha mwaka fedha 2020/2021, wakati ikiwasilishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya  Rais Ndg. Salum Maulid (hayupo pichani) kikao kilichofanyika katika  ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar.

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Issa Haji Gavu, akiwasilisha muktasari wa Ripoti ya  Utekelezaji Mpango9 Kazi wa Ofisi yake kwa kipindi cha mwaka wa fedha  2020/2021, kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibaer  (kushoto kwake) Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi  Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee  na ( kulia) Mshauri wa Rais Masuala ya  Ardhi,Nyumba Maji na Nishati Mhe. Burhan Saadat Juma.
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Ndg.Salum Maulid, akiwasilisha ripoti ya Utekelezaji Mpango Kazi kwa  mwaka wa fedha 2020/2021,kilichofanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini  Zanzibar.(kulia kwake) Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi  Seif Ali Iddi na (kushoto) Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Ndg. Salum  Kassim Ali.

MKURUGENZI Idara ya Mawasiliano Ikulu Ndg. Hassan Khatib,  akitowa maelezo wakati wa Kikao cha Utekelezaji Mpango Kazi kwa Kipindi  cha mwaka wa fedha 2020/2021. Kilichoongozwa na Rais wa Zanzibar na  Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein.(hayupo  pichani) kikao hicho kimefanyika katika ukumbi wa Ikulu Jijini  Zanzibar,17/8/2020.

WASHAURI wa Rais wakifufuatilia Kikao cha kuwasilisha ripoti  ya Utekelezaji Mpango Kazi kwa mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika  katika ukumbi wa Ikulu Jijini Zanzibar, wakati katibu Mkuu Ofisi ya Rais  Ndg. Salum Maulid, akisoma ripoti hiyo. (hayupo pichani).

MSHAURI wa Rais Masuala ya Historian a Mambo ya Kale Mhe.Ali  Mzee Ali, akichangia wakati wa Kikao cha Utekelezai Mpango Kazi kwa  mwaka wa fedha 2020/2021, kilichofanyika Ikulu Jijini Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Pages