August 20, 2020

RITA KUSOGEZA HUDUMA KARIBU NA MAKAZI YA WANANCHI

 

 Na Asha Mwakyonde

 
MPANGO wa usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwa watoto walio na umri wa miaka mitano (Underfive Birth Registration Program), umefanikiwa kwa kusajili zaidi milioni 5 na kupatiwa vyeti katika mikoa 18.
 

Mpango huo ni sehemu ya utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Usajili wa Matukio  muhimu ya Binadamu (Civil Registration and Vital Statistics (CRVS) strategy), ambao umeweza kupadisha idadi ya wastani wa watoto hao walio na vyeti vya kuzaliwa nchini kutoka asilimia 13 kwa mujibu wa senza ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 na kufikia asilimia 49.


Akizungumza jijini Dar es Salaam Agosti 20, mwaka huu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili Ufilisi na Udhamini (RITA), Emmy Hudson amesema mpango huo unalenga kuhakikisha kila mtoto aliye na umri chini ya miaka mitano anasajiliwa na kupata cheti cha kuzaliwa.
 

Mtendaji huyo amesema kuwa kila mtoto anayezaliwa anapata nyaraka hiyo ndani ya muda mfupi baada ya tukio la kizazi kutokea.
 

“Utekelezaji wa mpango huo unafanyika kwa kusogeza huduma karibu na makazi ya wananchi  kwa kutoa bila malipo katika ofisi za watendaji kata  na vituo vya tiba  vinavyotoa huduma  ya afya ya mama na mtoto, "amesema.
 

Amesema katokana na mpango huo Tanzania imeweza kutambulika kama moja ya nchi inayopiga hatua katika usajili wa vizazi na  kuchaguliwa kuwa kati ya nchi tano Barani Afrika  na pekee kwa Afrika Mashariki kuwasilisha mada kuhusu mikakati na mafanikio ya usajili huo yaliyopatikana kipindi cha mlipiko wa homa  kali ya mapafu (COVID 19).


Mtendaji huyo anasema Agosti 6, mwaka huu utekelezaji ulianza katika mikoa ya Kilimanjaro na Tanga  ambapo hadi sasa watoto zaidi ya 387,845, wamesajiliwa na kupata vyeti ambapo ni sawa na asilimia 66 ya watoto hao wanaotakiwa kusajiliwa.
 

“Utekelezaji wa mikoa yote Tanzania Bara unategemea kukamilika mwaka 2022 na kwamba mpango huo ni endelevu katika maeneo  ambayo umeanza kutekelezwa,“amesema Emmy.


Aidha amewataja wadau walioshiriki katika kufanikisha mpango huo kuwa ni Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF), serikali ya Canada na kampuni ya simu za mkononi TIGO pamoja na wadau wengine  muhimu wa masuala ya usajili na utambuzi wa wananchi.


Emmy amesema wadau wengine ni Ofisi ya Rais Tamisemi, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mamlaka ya vitambulishovya Taifa (NIDA),Idara ya Uhamiaji, Ofisi ya Taifa ya Takwimu.


Aidha amewataka wananchi katika mikoa hiyo tajwa waendelee kuitumia fursa hiyo  kuwapatia watoto vyeti vya kuzaliwa mara tu wanapozaliwa.
 

Naye Mkurugenzi wa Tehama Clife maligeli amsema kuwa mpango huo kwa sehemu kubwa unafanywa kwa njia ya kielekroniki na kwamba umeonyesha mafanikio.


Amesema huduma hiyo inafanya kwa njian ya simu  na kwamba mikoa ya Tanga na Kilimanjaro  tayari imefanikiwa kwa kuzajili zaidi ya  watoto 387,845  na kupatiwa vyeti.

No comments:

Post a Comment

Pages