August 19, 2020

VITALÓ FC YA BURUNDI KUTUA DAR IJUMAA TAYARI KUIVAA SIMBA J’MOSI

 

Haji Manara, Ofisa Habari Simba SC.

 

DAR ES SALAAM, TANZANIA

WAPINZANI wa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL), Simba katika pambano la Simba Day kuhitimisha Wiki ya Mabingwa 2020, VitalÓ ya Burundi, wanatarajia kutua jijini Dar es Salaam Ijumaa ya Agosti 21, tayari kwa mtifuano wao wa Jumamosi Agosti 22.

Wekundu wa Msimbazi chini ya Mbelgiji Sven Vandenbroeck, wako kambini kujiandaa na pambano hilo linalohitimisha wiki nzima ‘Champions Week’ ya utekelezaji wa miradi ya kijamii, kwa kuvaana na VitalÓ ya Burundi, baada ya kukwama kwa mipango ya kuleta timi za Afrika Kaskazini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, alisema: “Vital'O itafika Dar Ijumaa saa 5 asubuhi, ambapo jioni wageni wetu hao na sisi (Simba SC), tutafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa utakaotumika kwa pambano la Simba Day.

"Tulipanga kucheza na Al Ahly ya Misri Latina Simba Day 2020, lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tunaamini Vital'O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo,” alisisitiza Manara.

Mabingwa hao huitumia Simba Day kutambulisha nyota wapya kwa ajili ya kila msimu ujao, sambamba na jezi mpya za timu hiyo, inayojiandaa kutetea taji la VPL kwa msimu wa nne. Simba Day 2020 inaenda chini ya kaulimbiu ya #AnotherLevel #NguvuMoja.

Mapema wiki hii wakati akitangaza Wiki ya Mabingwa, Manara alisema tamasha lao litatumia viwanja vya Mkapa na Uhuru, na kuwa: “Uwanja wa Uhuru kiingilio kitakuwa ni Sh. 2,000, ambako kutakuwa na ‘big screen’ na wachezaji na benchi la ufundi wakifika wataenda kwanza kule kusalimia.”

No comments:

Post a Comment

Pages