September 03, 2020

Chuo Kikuu Mzumbe chawaalika wanafunzi kujiunga na chuo hicho

 
 
 
NA JANETH JOVIN

CHUO Kikuu Mzumbe, kimewaalika wanafunzi wote waliomaliza elimu ya Sekondari, cheti na diploma kuomba kujiunga na chuo hicho ili kupata taaluma iliyobora ambayo itawawezesha kujiajiri na kuajiliwa katika mashirika mbalimbali ya umma na binafsi.

Akizungumza katika maonesho ya 15 ya vyuo vikuu yanayoendelea katika viwanja wa Mnazi mmoja jijini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa lugano Kusiluka amesema, Mzumbe ni mojawapo ya vyuo vikuu vikubwa vya umma hapa nchini.

Amesema wamebobea katika utoaji wa kozi za utawala, uchumi, biashara, tehama, ujasiliamali hivyo anawataka wanafunzi kujitokeza kwa wingi kuja kusoma katika chuo hicho ili wawe wasomi bora.

"Unapozungumza nchi kuingia kwenye uchumi wa kati, unazungumzia utawala, biashara, sheria, ujasiliamali na mengineyo ambayo yote hayo tunayofundisha hapa chuoni kwetu, watu waelewe kuwa hayo ni mahitaji ya zamani hakuna mahali popote duniani unapoweza kuendesha uchumi bila ya kuwa na wataalamu wa fedha na wanasheria, biashara na wajasiriamali," amesema.

Aidha amesema Chuo hicho kimekuwa kikifanya maboresho katika matawi yake yote ambapo katika Tawi la Mbeya kunajengwa bweni litakalokuwa na unauwezo wa kuchukua wanafunzi 900.

" Kwenye kampasi kuu maboresho yanaendelea ambapo sasa tunajenga bweni linaloweza kuchukua wanafunzi 1000 ambalo tunatarajia mwishoni mwa mwaka huu litaanza kutumika kwani serikali iko katika hatua za mwisho kukamilisha.

Pia Chuo kiko katika hatua ya ujenzi wa madarasa mapya katika matawi yake yote yatakayoweza kuchukua wanafunzi ziada elfu moja, tunaboresha sana miundombinu katika Chuo chetu ili kiendane na umaarufu wa jina la Chuo hiki katika maeneo ambayo tunatoa huduma," esema.

Amesema, kuanzia mwaka huu Chuo hicho tawi lililopo Upanga ambalo kwa miaka mingi walikuwa wakitoa shahada ya uzamili (masters) sasa wataanza kutoa shahada ya kwanza.

Pia amesema, Chuo kupitia tawi la Dar es Salaam, wanajenga madarasa mapya eneo la Tegeta ma tunaomba wanafunzi kujitokeza kwa wingi na kujisajili ili waweze kupata elimu ya juu iliyo bora.

No comments:

Post a Comment

Pages