September 14, 2020

Kimei aiombea Himo kuwa Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda, akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge katika jimbo la Vunjo kupitia Chama cha Mapinduzi, Dkt. Charles Kimei katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika jimbo la Vunjo. Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Polisi Himo Septemba 12, 2020.

Maelfu ya wakazi wa Himo wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa kampeni wa chama cha Mapinduzi katika Jimbo la Vunjo Uzinduzi huo ulifanyika katika viwanja vya Polisi Himo Septemba 12, 2020.  

 

 

Himo, Kilimanjaro.

 

 MGOMBEA Ubunge wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Jimbo la VunjoMoshi Vijini, Dkt. Charles Kimei  amewaomba wananchi wa Jimbo hilo kumpa ridhaa ya kuwa Mbunge wao ili aweze kuwaletea mapinduzi ya kiuchumi. Aliyasema  hayo katika Mkutano wa uzinduzi wa kampeni zake  uliofanyika katika Mji mdogo ya Himo na kuratibiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Pinda na  kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Jimbo hilo.

 

Katika hotuba yake, Dkt. Kimei alisema  kuwa Jimbo hilo lina changamoto nyingi ikiwamo miundombinu mibovu ya barabara, Elimu, Afya na ukosefu wa masoko thabiti kwa mazao yazalishwayo na wakazi wa jimbo hilo.

 

Alisema kuwa, ikiwa wananchi watamchagua kuongoza jimbo hilo, atatumia uzoefu wake katika sekta ya Fedha, kuanzisha Mfuko wa Ujasiliamari wa Jimbo ambao utahusika kutoa mikopo nafuu kwa wanachi ili kuwapa mItaji na hivyo kuwajengea uwezo wa kujiajiri na kuajiri ili kuwapaisha kiuchumi. “Kwa kushirikiana na wadau wengine, tunakamilsha mchakato wa kuanzisha mfuko wa Wajasiliamari Vunjo. 

 

Mimi mwenyewe nitatoa andiko la mradi  yaani (Project write-up) ili kupata fedha za uwezeshaji wa makundi maalum ya Wakulima, Wafugaji, Vijana, Wanawake, Bodaboda  na mafundi makenika kwa kuwapa mikopo nafuu”.

 

Kuhusu Kilimo na mazao ya shamba, Dokta Kimei alizungumzia kuhusu kuanzishwa Kilimo cha umwagiliaji ili kuongeza tija, sambamba na kuwawezesha wananchi kuanzisha viwanda vya usindikaji hivyo kuongeza thamani ya mazao. Jambo kubwa la msingi ni kuanzisha viwanda vya usindikaji ili kuongeza thamani ya mazao yetu. Badala ya kuuza Mpunga, tutaanza kuuza mchele wetu uliofungwa vizuri. Badala ya kuuza nyanya ambazo huharibika kirahisi, viwanda hivi vitasindika nyanya hizo na tutauza Tomato paste yetu wenyewe hivyo kuongeza thamani na vipato vya wananchi wa Himo. Tutafanya hivyo pia kwa mazao ya Kahawa na mengineyo’ alisema Dkt. Kimei.

 

Aliongeza kuwa, eneo lingine ni kuboresha miundombinu ya Barabara ili kurahisisha usafarishaji wa mazao hayo ili kufikia masoko kwa urahisi  kutokana na hali hiyo, maisha ya wananchi yatabadirika na kupiga hatua za kimaendeleo.

Kwa upande wa changamoto sekta  ya afya, Dkt. Kimei alisema kuwa vituo vingi vya afya vinahitaji ukarabati mkubwa wa haraka huku vikikosa vifaa vya kisasa kama XRAY na Ultra sound. “Tutasimamia kukamilisha ujenzi wa hospitali wa wilaya ya Himo ambao ulisimama. Pia tutashughulikia masuala ya Bima za afya na matibabu kwa Wazee. Kuhusu ukosefu wa gari la Wagonjwa, Dokt. Kimei alisema ‘Kwa sasa, Jimbo letu halina gari la uhakika la kubebea wagonjwa, Naahidi kutoa gari  langu mimi mwenyewe, lifanye kazi hiyo wakati tunaendelea na mchakato wa kuongeza mengine”alisema.


"Nimejipanga kuhakikisha wananchi wa 
Himo wanapata maendeleo kama inavyosema ilani ya Chama cha Mapinduizi. Nitashirikiana na Serikali kila nyanja ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kunufaika na rasilimali zao." alisema Dkt. Kimei


Aidha, pia
 Kimei mbali ya kujiombea kura, pia aliweza kumuombea kura nyingi na za kishindoi kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na Madiwani wote wa CCM ndani ya jimbo hilo la Vunjo. 

No comments:

Post a Comment

Pages