NA JANETH JOVIN
Mgombea Mwenza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Samia Suluhu Hassan amewataka wagombea wa nafasi mbalimbali walioshindwa katika Jimbo la Kigamboni kuacha nongwa bali warudi kunduni na kuungana kwa pamoja kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi.
Mama Samia amesema yeyote atakayebainika kuwa anakihujumu chama kwa kuzunguka mitaani basi hatachukuliwa hatua na kusisitiza kuwa chama hicho kipo macho na kitamtambua mtu huyo atakayefanya hujuma.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika Viwanja vya Mjimwema Kigamboni wakati wa muendelezo wa kampeni zake, Mama Samia amesema wale wote walioshindwa katika kura za maoni Kigamboni anawaomba kundini na endapo wakigundua kuwa wanafanya nongwa au kukihujumu chama basically watakula saa moja na yeye.
Amesema mashikamano katika uchaguzi ni kitu muhimu na endapo wanachama wataruhusu wagawanyike basi wapinzani watashinda kirahisi uchaguzi Mkuu.
"Tusijaribu kuruhusu jambo hilo, najua wanaKigamnoni mpo imara hivyo tushikamane na kwa umoja wetu twende tukapige kura na hatimaye tupate ushindi," amesema.
Amesema katika jimbo hilo la Kigamboni ndani ya miaka mitano ijayo watakomesha tatizo la ukosefu wa maji ya Dawasa na kuongeza kuwa wataendelea kujenga hospitali na kusambaza umeme vijijini.
Aidha Mama Samia amesema kuwa katika miaka mitano ijayo watatekeleza mradi maalum wa kukomesha tatizo la mafuriko eneo la Jangwani jijini Dar es Salaam.
"Tutaendelea kukarabati miundombinu ya elimu na kuhimarisha elimu ya watu wazima, hakika kote nilipopita katika jiji la Dar es Salaam nimeona yamefanyika mambo makubwa, hakuna kitu ambacho tuliahidi hatujakifanya bali vipo vilivyoanza kujenga na tukipewa mingine mitano tutamalizia, " amesema
Naye mgombea ubunge Jimbo hilo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile amesema katika kipindi cha miaka mitano mambo makubwa yamefanyika Kigamboni kwani kwa sasa umeme kwenye jimbo hilo haukatiki ovyo.
Amesema katika miaka mitano ijayo watahakikisha Kigamboni inakuwa eneo la viwanda litakalotoa ongeza idadi ya ajira kwa Vijana na kuongeza kuwa wameshatenga Bilioni 75 kwa ajili ya kujenga soko la samaki Pemba Mnazi.
"Wananchi wa Kigamboni mlinipa imani yenu na mimi nawaahidi kuwapatia maendeleo, hakikisheni mnaichagua CCM ili kuleta maendeleo ya kweli," amesema
No comments:
Post a Comment