September 07, 2020

Waandishi wa habari, watumiaji wa mitandao ya kijamii waaswa kufuata sheria, taratibu

NA JANETH JOVIN

SHIRIKA lisilo la Kiserikali la Paradigm Initiative Afrika limewataka watumiaji wa mitandao ya kijamii kuitumia Kwa usahihi hasa kwa kufuata sheria na taratibu zilizowekwa na nchi kupitia mamlaka husika.

Aidha shirika hilo limewataka waandishi wa habari pia kufanya kazi zao Kwa kufuata taratibu zilizoweka na mamlaka husika zinazowasimamia ili wananchi kupata habari bora zenye weledi.

Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Mratibu wa Shirika hilo, Peter Mmbando wakati wa majadiliano yaliyowakutanisha waandishi wa habari na watetezi wa haki za binadamu kwa lengo la kujadili sheria ya mitandao Kwa Tanzania hususani katika uhuru wa vyombo vya habari na kuangalia namna ya kusaidia kuboresha ufanisi,  bora ya upashaji  habari .

Akizungumza katika majadiliano hayo, Mmbando amesema katika kipindi hiki cha uchaguzi waandishi wa habari wanatakiwa kuandika habari kwa kufuata sheria ili kulinda haki za wananchi za kupata habari sahihi na zenye uhakika.

Aidha amesema watumiaji wa mtandao ya kijamii wanapaswa kuitumia kwa usahihi hasa kwa kufuata sheria ya mamlaka husika

“Nawaasa  kufuata taratibu ambazo zimewekwa na mamlaka husika ili kulinda haki za wananchi katika  kuwapasha habari,Habari zinatakiwa ziwe za kweli hazitakiwi ziwe fake,”amesema.

Aliongeza kuwa mtu anapodanganya jamii kwa sauti/video anaharibu taratibu uliowekwa kisheria.

Hata hivyo Mmbando amesema yapo makundi ambayo hayajasomea mambo ya habari, wanatakiwa kuacha kutoa taarifa ambazo hazina ukweli na kupotosha umma ni kuharibu utaratibu za mamlaka.

Kwa upande wake Ice Erick kutoka shirika  masuala ya umoja, Amani na maendeleo(OPCB), amesema kupitia mkutano huo wamejifunz amambo mengi yanayo husu matumizi sahihi ya mitandao.

Amesema  changamoto za matumizi ya kimtandao ni jukumu lao  kuhakikisha watu ambao wanaweza kupata maafa kutokana na matumizi yasiyosahihi.

“Nadhani inaweza kuwa hatua nzuri kwa sasa kuiga mfano kwa nchi zingine kama jambo litakuwa na matokeo mazuri kutoka nchi zingine kuweza kulinda uhuru wa matumizi ya mtandao,”amesema.

Hata hivyo mmoja wa mshiriki wa mkutano huo, Kenedy Mmari amesema majadiliano hayo  muhimu hasa katika kushirikisha wadau katika michakato mbalimbali ya uundaji wa sera na sharia inayosimamia sekta mbalimbali ikiwemo  mawasiliano ya kimtandao na vyombo vya habari.

“Katika miaka ya hivi karibuni sheria nyingi zenye mlengo mzuri  zinazingatia habari sahihi mtandaoni, usimamizi mzuri wa mtandaoni lakini sababau za msingi kunapokuwa hakuna msimamizi wa habari za ukweli inaleta athari,”amesema.

Amesema kuletwa kwa mapendekezo ya sheria hizo kulionekana kwa changamoto zake huku kukiwa na kilio kwa wamiliki kutokana na gharama za usajili kuwa mkubwa kama blog, televisheni mtandao.

Aliongeza kuwa jambo hilo linaathiri vijana ambao walitaka kujiajiri kwa kuweka maudhui mtandaoni.

No comments:

Post a Comment

Pages