September 15, 2020

Waliofanya vizuri masomo ya sayansi wapewa tuzo


NA ASHA MWAKYONDE

 
KATIBU  Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto profesa Mabula Mchembe amelitaka Baraza la Mitihani Tanzania NECTA kutoa mwendelezo wa taarifa za wanafunzi wanaofanya vizuri kitaifa hata baada ya kumaliza masomo yao yote  elimu ya juu ili kusaidia kujua maendeleo yao na mchango wao katika ujenzi wa Taifa.


Akizungumza  jijini Dar es Salaam Septemba 14, mwaka huu wakati wa ghafla ya utoaji tuzo za wanafunzi na waalimu bora kitaifa  mwaka 2018 na 2019 katika masomo ya kemia,fizikia na baoilojia kidato cha nne na sita iliyoandaliwa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa serikali, amesema  kuna umuhimu wa kujua maendeleo ya vinara hao hata baada ya kumaliza masomo.


Mchembe ameshauri  shule kuongeza jitihada za kuboresha mazingira ya kusomea wanafunzi ikiwemo maabara za kujifunzia kwa kuhakikisha vifaa na kemikali zinazohitajika zinakiwepo za kutosha ili wanafunzi waeweze kusoma kwa vitendo zaidi na zaidi na idadi ya wanaofaulu kwa kiwango
cha juu kuongezeka.
 

Naye Mkemia mkuu wa serikali Dkt. Fedelice Mafumiko amesema  toka kuanza kwa tuzo hizo mwaka 2007 mpaka sasa wameshatoa tuzo kwa wanafunzi 288 na waalimu 22,ambapo utoaji wa zawadi hizo umekuwa ukiongeza moralali kwa wanafunzi na waalimu kuendelea kufanya vizuri
zaidi.


Amesema kuwa wanafunzi waliotunukiwa tuzo ni 36 na walimu wao 6 hivyo kufikisha jumla ya wanafunzi 288 na walimu 22 tangu kuanza kwake.


Dkt. Mafumiko amesema kuwa lengo la utoaji tuzo hizo kwa masomo hayo ni kuwashawishi wanafunzi wengi kupenda masomo ya sayansi ili kusaidia taiafa kutatua changamoto za majanga mbalimbali yanayotokea ikiwamo la ajali ya moto, maji. "Niwahakikishie wananfunzi mliotunukiwa tuzo za vyeti siku hii ya leo ni kumbukumbu tosha ya historia ya taalamuma zenu muendelee kuongeza juhudi ya kusoma kwa bidii mfike mbali  "amesema Dkt. Mafumiko.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi wa mamlaka ya mkemia mkuu wa serikali   Profesa Hellen  Jason amewahimiza watoto wakike kusoma masomo ya sayansi na kuondokana na kasumba iiyopo jamii kuwa masomo hayo ni magumu huhusani kwa mabinti. 

"kumekuwa na kasumba kubwa sana kwa jamii kuwaambiwa wanafunzi wa jinsia ya kike kuwa hawawezi kusoma masomo ya sayansi ni magumu kufaulu kwa ni vigumu mimi nasema kasumba hiyo iondoke mara moja wanawake wanaweza kusoma masomo ya sayansi, "amesema Profesa Heleni.


Kwa upande wake mwananfunzi wa shule ya sekondari Tabora aliyemalizwa mwaka jana na kushika nafasi ya nne kitaifa kwa wasichana Vanesa Mtabana amesema kufanya vizuri ni kutokana na juhudi za mtu binafisi
na sio shule.
 

Amesema anashukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwekeza zaidi katika elimu ambapo hadi sasa shule za serikali zinafanya vizuri. "Walimu pia wanamchango mkubwa katika kusukuma maendeleo ya wanafunzi kimasomo kwani juhudi na matunda yao zinaonekana, " amesema Vanesa.

No comments:

Post a Comment

Pages