Na Mwandishi Wetu
KANISA
la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Boko limekabidhi
vifaaa mbalimbali vya matibabu kwa Hospitali ya Taifa ya Muhumbili
kitengo cha Watoto wenye Ugonjwa wa saratani.
Akikabidhi
vifaa hivyo Mchungaji wa Kanisa hilo, Ambakisye Lusekelo, amesema
wamekabidhi vifaa ambavyo vitatoa msaada wa kimatibabu kama ambavyo
Ungozi wa Muhimbili ulitoa Muongozo huku akiwatakia heri na amani katika
huduma wanazozipata.
"Tupo kwa ajili ya
matendo ya huruma ya kusaidiana, tunaomba Mungu sana aendelee kuwanganga
na kuwaponya lakini awatie nguvu na kuwatia moyo na kuwapa amani wazazi
na walezi ambao wanawahudumia, Madakatari wetu pia tunawakabidhi
mikononi mwa Mungu azidi kuwapa upendo kwa watoto hawa.
"Damu
ya Yesu ikiambatana na vifaa hivi tulivyovileta itakwenda kuwaponya
hawa watoto, kufika kwetu hapa ni kwa ajili ya nguvu na uweza wa Mungu
mwenyewe kwamba kwa njia ya matendo ya huruma, Yesu akawakumbuke watoto
wetu Ameen."amesema Lusekelo
Baadhi ya wakinamama wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kukabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 katika wodi ya watoto ya wagonjwa wa saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Mwenyekiti wa Kwaya ya Umoja wa Wanawake Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Mama Lema (kushoto) na Mama Milen wakielekea katika Wodi ya Upendo kukabidha vifaa tiba.
Baadhi ya walezi na wazazi wakiwa katika picha ya kumbukumbu na akinamama wa Umoja Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko
Maelekezo.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Ambakisye Lusekelo, akiongoza maombi kabla ya kukabidhi vifaa tiba.
Mzee wa Kanisa Ruth Mloge, akisoma neno la Mungu.
Katibu Msaidizi Umoja wa Wanawake KKKT Usharika wa Boko, Prisca Ndambala, akisoma neno la Mungu.
Mwenyekiti wa Kwaya ya Umoja wa Wanawake KKKT Usharika wa Boko, Mary Lema, akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa tiba.
Mweka Hazina wa Msaidizi wa Umoja wa Wanawake wa KKKT-Boko, Magdalena Nyellah, akifafanua jambo wakati wa kukabidhi vifaa tiba katika Wodi ya Upendo na Tumaini
Muuguzi katika wodi ya Tumaini, Asteria Henjewele, akizungumza wakati wa kupokea vifaa tiba kutoka kwa kikundi cha Umoja wa Wanawake wa Kanisa la KKKT Usharika wa Boko jijini Dar es Salaam.
Kukabidhi chandarua.
Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Boko, Ambakisye Lusekelo, akikabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba kwa wauguzi wa wodi ya Watoto wanaougua saratani katika hospitali ya Taifa Muhimbili.
No comments:
Post a Comment