Wauguzi na Wakunga nchini wametakiwa kuepuka kutoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa na kwani kwa kufanya hivyo ni kinyume na maadili na miiko ya taaluma hiyo.
Hayo yameelezwa Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi huduma za Uuguzi na Ukunga kutoka Wizara ya Afya, amaendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ziada Sellah wakati wa kikao kazi na Wauguzi na Wakunga Mkoa wa Dar es Salaam.
Sellah amesema kumekuwa na tabia chafu ya baadhi ya Wauguzi na Wakunga kujikuta wanatoa lugha zisizofaa kwa wagonjwa jambo linaloweza kuharibu taswira ya taaluma hiyo.
Aidha Ziada ametoa wito kwa Wauguzi kujiendeleza kielimu ili waweze kujiongezea maarifa na utaalamu wa kutoa huduma Bora na zenye tija kwa wagonjwa.
Pamoja na hayo amewaasa watumishi wa sekta ya Afya kufanya kazi kwa Umoja na Mshikamano huku wakizingatia suala la uwazi.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Dk. Rashid Mfaume na Mkurugenzi wa huduma za Uuguzi na Ukunga Mkoa wa Dar es salaam wametoa wito kwa Wauguzi kuheshimiana na kuthaminiana katika mazingira ya kazi.
Mkurugenzi huduma za Uuguzi na Ukunga Kutoka Wizara ya Afya yupo Dar es Salaam kwa ziara ya kikazi ya siku mbili kwenye Hospital mbalimbali za Mkoa huo kwa lengo la kujionea shughuli mbalimbali za kiuuguzi na kuzungumza na Wauguzi lengo likiwa ni kuongeza ufanisi wa kazi.
No comments:
Post a Comment