October 06, 2020

ZITTO KABWE APATA AJALI


Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ndugu Zitto Kabwe amepata ajali ya gari akiwa njiani akitokea Kata ya Kalya kuelekea Lukoma kwenye kampeni katika Jimbo la Kigoma Kusini leo Jumanne Oktoba 6, 2020.


Zitto alikuwa na watu  watano kwenye gari yake na wote wako salama ingawa wamepata majeraha na wanahisi maumivu makali.


Wamepata huduma ya kwanza kwenye eneo la ajali baadaye wamepelekwa Kituo cha Afya cha Kalya kilichopo Wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma.


Imetolewa na:

Arodia Peter

Afisa Habari ACT-Wazalendo

Oktoba 6, 2020

No comments:

Post a Comment

Pages