November 08, 2020

Mikoa minne kupata mvua kubwa

Mkurugenzi Mkuu TMA,  Dk. Agnes Kijazi.

Na Irene Mark


MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa tahadhari ya uwepo wa mvua kubwa kwa 
baadhi ya maeneo ya Kaskazini mwa pwani ya Bahari ya Hindi kwenye mikoa minne.

Tahadhari hiyo imetolewa leo Novemba 08.2020 na kwamba mikoa itakayohusika ni Dar es salaam, Morogoro, Tanga na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia, Unguja na Pemba.

Kwa mujibu wa taarifa ya TMA kwa vyombo vya habari, imeeleza kwamba mvua hizo zitanyesha kwa siku tatu kuanzia leo Novemba8. 

“Uwezekano wa kutokea kwa mvua hizo ni wastani hivyo athari zinazoweza kujitokeza ni mafuriko kwenye makazi, baadhi ya barabara kufungwa na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi.

“Tunawashauri wakazi na mamlaka zinazohusika kwa mikoa hiyo wachukue tahadhari za kutosha kudhibiti athari zinazoweza kutoka,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages