WAKATI
kukiwa na hofu ya kuwepo kwa matumizi ya mbegu za mazao ambazo
zinatokana na Mbegu Zilizoongezewa Vinasaba (GMO) Serikali imesema bado
haijaruhusu matumizi ya mbegu hizo hapa nchini kwa ajili ya uzalishaji
ila kwa sasa kinachoendelea ni utafiti.
Hayo
yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira),
Joseph Sokoine, wakati akifungua kongamano la wazi la kujadili usalama wa
mbegu lililoandaliwa kwa pamoja kati ya Taasisi Mwamvuli ya Kilimo Hai
Tanzania (TOAM) na Shirika linalojishughulisha na Baionuwai nchini
(TABIO).
Katika kongamano
hilo ambalo lilishirikisha wadau zaidi ya 300 kutoka nchi tano za
Afrika Kusini, Bokinafaso, Ivory Cost, Tanzania na Uswisi Naibu Katibu
Sokoine amsema taarifa za kuwepo matumizi ya mbegu za GMO zinapaswa
kupuuzwa Kwani hazina ukweli ila utafiti unaendelea.
Amesema
Serikali haina sababu ya kuficha taarifa iwapo kuna mbegu zinazotokana
na GMO hivyo kuwaomba wadau kutoa taarifa iwapo wana ushahidi wa kuwepo
mbegu hizo.
"Utafiti
mbegu hizi za GMO unafanyika katika shamba letu la Makutopora Dodoma,
hatuzalisha ila zipo kwa ajili ya utafiti, Serikali lazima tujiridhidhe
kabla ya kuruhusu kutumika au kutotumika naomba mmpuze taarifa kuwa
mbegu hizo zinatumika," amesema Sokoine.
Amesieitiza kuwa Tanzania kuna Sera ambayo inatambua teknolojia ya inayoleta maendeleo kwenye kilimo lakini pia Sera inayotambua kilimo endelevu hivyo ni jukumu la wadau kwenda pamoja kwa maslahi ya nchi na wananchi.
Sokoine amesema uwepo wa mijadala kama hiyo juu ya usalama wa mbegu itasaidia kwa kiasi kikubwa kuona njia sahihi ya kuifuata katika utunzaji na uwendelezaji wa mbegu kwa ajili ya kizazi cha sasa na kizazi kijacho.
Naibu
Katibu Mkuu huyo amesema Serikali inapenda kuona taasisi kama TOAM na
TABIO kuleta mijadala ambayo inagusa maisha ya Watanzania.
Mkurugenzi Msaidizi wa maendeleo ya mazao kutoka Wizara ya Kilimo, Beatus Malema, amesema Serikali inaunga mkono kilimo endelevu nchini (Kilimo hai) na kuwataka watu kuwekeza kwenye pembejeo ili kuongeza tija ya uzalishaji.
Malema amesema kilimo hai kinatunza ardhi jambo ambalo litapunguza kama sio kuondoa matumizi ya kemikali wakati wa msimu wa kilimo ili kuongeza uzalishaji.
"Tunatambua
mbegu za asili ndio chanzo cha mbegu zote zikiwemo zinazobadilishwa
vinasaba hivyo kuna haja kubwa ya kuzitunza kwa ajili ya vizazi vijavyo
lakini pia zinachochea uzalishaji msingi," amesema.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa TOAM, Dk. Mwatima
Abdallah Juma akizungumzia kongamano hilo amesema kuwa duniani kwa sasa
kuna msukumo mkubwa wa matumizi ya GMO hali inayohatarisha usalama wa
mbegu za asili hivyo ni jukumu la wadau wa kilimo hai kuungana na
Serikali kupinga mbegu hizo kwa kuwa sio salama kwa mlaji.
Dk.Juma amesema kongamano hilo litatoa nafasi kwa wakulima kuona umuhimu wa mbegu za asili na zinazoitwa za GMO.
"Sisi
tunaamini mbegu za asili ndio suluhisho la kuongeza uzalishaji zaidi
kama watu watafuata kanuni za kilimo bora na kilimo endelevu pamoja na
kuwa kila mkulima ana chaguo lake," amesema Dk Juma.
Wakichangia
katika kongamano hilo lililofadhiliwa na Ubolozi wa Ufaransa na Uswisi
baadhi ya wadau wa kilimo waliweka wazi kuwa kilimo salama na endelevu
ni kutumia mbegu asili.
Wamesema
dunia inapaswa kuwa kauli moja katika suala la mbegu na kilimo kwani
sekta hiyo ni muhimu kwa maendeleo, kiuchumi, kisiasa na kijamii.
"Kukiwa
hakuna usalama wa mbegu ni wazi kuwa hata wa chakula hautakuwepo hivyo
ni jukumu la wadau wote kuwa pamoja katika kupigania mbegu asili,"
amesema mdau mmoja wa kilimo.
No comments:
Post a Comment