Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa mradi wa ASCEND.
Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo, akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
Na Asha Mwakyonde
MAMLAKA
ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imezindua mradi wa ASCEND wa miaka miwili
na nusu unaolenga kudhibiti mifumo ya majaribio ya dawa kwa binadamu
na tafiti mbalimbali zinazofanyika nchini.
Akizungumza jjijini Dar es Salaam leo mara baada ya kuzindua mradi huo Mganga Mkuu wa Serikali Prof. Abel Makubi amesema ASCEND itawasaidia TMDA kuhakikisha majaribio ya dawa kwa binadamu nchini inakuwa kwa viwango stahili
Amesema
kama kipimo kikionyesha kuwa na uwezo wa kugundua maradhi,mradi huo
utakuwa chachu kwa TMDA kuondoa baadhi ya changamoto katika shughuli
zake,ikiwemo kuchelewa kutolewa majibu haraka za majaribio ya dawa
zinazofanyika nchini”amesema.
"Na matokeo ya majibu yanayotarajiwa Kama ni dawa ikaonekane ina uwezo wa kutibu binadamu,"amesema mganga huyo.
Prof.
Makubi amesema kuna haja ya TMDA kuangalia gharama zinazotozwa hasa kwa
wanafunzi wanaofanya majaribio ya dawa ikiwa ni sehemu ya masomo yao
kwani wamekuwa wakipitia changanmoto nyingi kumudu gharama zilizopo.
Makubi
amesema Serikali imeukubali mradi huo na iko tayari kuwasaidia lakini
wahakikishe tafiti zote za majaribio ya kitabibu zinadhibitiwa vizuri na
kwa viwango vya juu vinavyostahili na kutoa majibu yanayotarajiwa.
Hata
hivyo Prof. Makubi ametoa wito kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Nchini
TMDA kuwa inatakiwa kuwajengea usezo watafiti ambao bado ni vijana kwani
baadae watakuja kusimamia na kuhakikisha majaribio ya kitanibu
matunda yanaonekana.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo alisema utekelezaji wa
mradi huo, utawasaidia kwa kiwango kikubwa kuboresha mifumo ya
dawa,namna ya kupitisha maombi ya dawa kabla ya kufanyika nchini na
kuweka mifumo bora itakayofuatilia watumiaji wa dawa za majaribio.
“Tutaweka
mfumo ambao utahakikisha wote wanaotumia dawa za majaribio wanakuwa
salama muda wote na kuwatunza wote wanaoshiriki katika majaribio ya
dawa”amesema.
Fimbo
amesema kupitia Chuo Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili
(MUHAS)kupitia mradi huo mafunzo yatatolewa wanaofanya utafiti ili kuwa
na uelewa mpana juu ya masuala ya utafiti
Ameongeza kuwa mradi huo unahusisha Tanzania bara na visiwani,lengo likiwa ni kuleta wataalamu waliobobea.
Mkurugenzi
huyo amesema mradi huo umehusisha taasisi saba ikiwemo MUHAS ,Taasisi
ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR),Mamlaka ya Chakula na Dawa
Zanzibar (ZFDA) ,Chuo kikuu cha St Andrews ya Scotland Taasisi ya
Utafiti Kilimanjaro (KCRI).
"Mradi huu umehusisha taasisi kutoka nchi zilizoendelea, ikiwa ni utaratibu uliopo katika taasisi ya kimataifa EDCPT, amesema.
EDCPT
ambayo ndio wafadhili wa mradi huo kwa miaka miwili na nusu hutoa
fedha kwa nchi zinazoendelea na zilizopo bara la Ulaya kwaajili ya
kusaidia tafiti mbali mbali ikiwemo uboreshaji wa mifumo hasa udhibiti
wa majaribio ya dawa.
Naye
Afisa Utafiti kutoka Taasisi ya UItafiti Afya Zanzibar (ZAHRI) Hamis
Rashid Kheri amesema mradi huo utaisaidia Tanzania kufanya tafiti .
No comments:
Post a Comment