Kampuni ya simu za Mkononi Airtel Tanzania leo imetangaza
kuzindua ofa ya Airtel Smartphone Dabo Data kwa wateja wote wa simu aina
ya Smartphone kwa msimu huu wa sikukuu.
Pia ofa hii
itawanufaisha Wateja wote wa sasa wa Airtel wanyempango wa kubadilisha
simu au Smartphone mpya kwa kujipatia Dabo Data kwa bando za wiki na
mwezi kwa miezi sita ijayo yaani nusu mwaka.
Airtel inapozindua
Ofa hii ya shamrashamra za mwisho wa Mwaka Wateja wengine wa smartphone
kwa sasa wanaweza kujiunga na mtandao wa Airtel ili kufurahi ofa hii.
Ofa hii ni pale mtu mtumiaji wa simu aina ya smartphone anapotumia
mtandao wa Airtel kwa mara ya kwanza kwenye simu yake. Ofa hii inatoa
fursa kwa wateja kufurahia huduma yenye kasi ya Airtel 4G inayopatikana
nchini kote Tanzania.
Ofa ya Dobo Data inampa mteja mara mbili
kwa kila bando analonunua ikiwa ni ya wiki au mwezi kwa kipindi cha
miezi sita yaani Nusu Mwak. Ili kujipatia ofa hii, mteja wa smartphone
anatakiwa kupiga *149*99#, changua 5 (intaneti) kisha 6 (Smartphone ofa)
ili kujiunga. Baada ya kujiunga kikamilifu, mteja atapata ofa mara
mbili ya bando lolote atakalo nunua iwe ni kwa siku saba au mwezi kwa
miezi sita ijayo kuanzia siku ambayo amejiunga.
Muda wa ukomo wa
Airtel Smartphone Dabo Data ni sawa na ule ambao bando imenunuliwa na
bonasi ya data kwa wale tu waliojiunga na ofa hii.
Ezekiel
Kahatano, Mkuu wa kitengo cha Data na Masoko Airtel Tanzania anasema,
“Dhamira yetu siku zote ni kuwapa wateja wetu huduma bora ambayo
inaendana na Maisha ya sasa ya kidigitali. Kwa maana hiyo, leo
tunatangaza kuzindua ofa ya Airtel Smartphone Dabo Data, ambayo inawapa
wateja unafuu kwenye kupata huduma bora ya Airtel 4G. Wakati tunakaribia
msimu wa sikukuu, hii itawapa wateja wetu fursa ya kuendelea
kuunganishwa na familia, marafiki na wadau wote kote nchini.
Kwa upande wake, Meneja Mawasiliano Airtel Tanzania Jackson Mmbando anasema;
“Ninachukua fursa hii kuwaomba wateja pamoja na watumiaji wa smartphone
kujiunga na mtandao wa Airtel ili kufurahi ofa hii kwa WIKI na MWEZI
kwa bando za intaneti kwa Nusu Mwaka. Tunaamini ya kwamba wakati wa
kipindi hiki cha msimu wa sikukuu wateja wetu wanahitaji uhuru wa
kuwasiliana na marafiki, familia na wafanya biashara wenzao na kwa hivyo
huduma hii inawapa uhuru ule wanaohitaji”.
Kuzindulia kwa ofa
hii ya Smartphone data ambayo inampa bonua ya asilimia mia moja mteja
inaonyesha ni kwa kiwango ngani tunavyothamini wateja wetu. Tuna Imani
kuwa huduma hii itawapa hamasa wale ambao sio watumiaji wa smartphone
kuanza kutumia na hivyo kukuza Maisha ya kidigitali kwa Watanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Data kampuni ya Simu za mkononi, Airtel, (kulia) na
Meneja Mawasiliano wa Kampuni hiyo, Jackson Mbando wakizindua rasmi Ofa
ya Siukuu kwa wateja kwa kuwapa Dabo Data.
December 01, 2020
Airtel Yaja na Ofa ya Sikukuu Wateja Kupewa Dabo Data
· Wateja wa Airtel Smartphone kupata Dabo Data kwa Nusu Mwaka.
No comments:
Post a Comment