Kiongozi wa Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao ya
Misitu (FORVAC), Juhani Harkonen akiangalia gogo lilikatwa kwa ajili ya
mbao katika Kijiji cha Sautimoja wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Msitu ukiwa umependeza kutokana na utunzaji unaoafanywa na wananchi wanaouzunguka.
NA SULEIMAN MSUYA
WATANZANIA
wameshauriwa kutunza rasilimali misitu kama wanavyotunza familia zao
kwa kuwa ina faida nyingi kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Ushauri
huo umetolewa na Kiongozi wa Program ya Mnyororo wa Thamani wa Mazao
ya Misitu (FORVAC), Juhani Harkonen katika mahojiano maalum na mwandishi
wa habari hii jijini Dar es Salaam.
FORVAC
ni program inayotekelezwa kupitia Idara ya Misitu na Nyuki chini ya
Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland
kuhakikisha misitu inachangia huduma za kijamii, uchumi na utunzaji
mazingira.
Program hiyo inatekelezwa katika wilaya 12 ambazo ni Tunduru, Namtumbo, Nyasa, Mbinga na Songea zilizopo Kongani ya Ruvuma.
Kongani
ya Lindi ina wilaya za Nachingwea, Ruangwa, Liwale na Kongani ya Tanga
ina wilaya za Handeni, Kilindi, Mpwapwa na Kiteto.
Harkonen
amesema ili misitu iweze kuwa endelevu ni vema kila mwananchi
akachukulia kwa mtazamo chanya kwa kupanda na kuilinda ili iweze
kuchangia ukuaji wa uchumi na maendeleo yao.
Amesema
nchini Finland misitu ina thamani sawa na nyumba, familia na vitu
vingine muhimu hali ambayo inachochea uhifadhi shirikishi na kuitunza.
"Nitumie
nafasi hii kuwaomba Watanzania kuchukulia misitu kwa uzito mkubwa kama
wanavyofanya kwa familia na mali zao kwani ni rasilimali muhimu sana kwa
jamii kiuchumi, maendeleo na mazingira," amesema.
Kiongozi
huyo wa FORVAC amesema Serikali kwa kushirikiana na wadau ina wajibu wa
kutoa elimu kuanzia elimu ya msingi ili kila mmoja aweze kushiriki
kutunza misitu.
"Jambo
lolote ili lifanikiwe linahitaji elimu na sisi katika hizi wilaya 12
ambazo tupo tumeanza na elimu kwanza hali ambayo inarahisisha
utekelezaji," amesema.
Harkonen
amesema katika vijiji ambavyo vinashiriki program wamehakikisha kuna
mpango wa matumizi bora ya ardhi ili kuepusha migogoro.
Amesema
FORVAC inaamini rasilimali misitu ikitumika kwenye mfumo wa Usimamizi
Shirikishi wa Misitu ya Jamii (CBFM), itakuwa salama na endelevu na
kuinua maisha yao.
"Misitu
ikitumiwa kwenye mfumo wa CBFM ina uwezo wa kubadilisha maisha ya
wanayoizunguka na nchi kwa ujumla na uhakika wa uendelelevu utakuwepo,"
amesema Harkenon.
Aidha,
kiongozi huyo amesema pamoja na kuhamasisha CBFM ni muhimu sheria, sera
na kanuni za misitu ziendane na wakati husika kwa maslahi ya nch.
Amesema kiujumla FORVAC imeona mafanikio ya miaka miwili ya program hiyo jambo ambalo linawapa nguvu kushawishi kuendelea.
Mtaalam
Kijana wa Kimataifa Anayeshughulikia Ufuatiaji na Thamini wa Mradi,
Nette Korkanen amesema mwitikio wa wanavijiji ambao wanatekeleza program
hiyo ni mzuri jambo linaloleta matumaini.
"Sisi
kwetu Finland tumekuwa tukiamini misitu ni muhimu na ina faida hivyo
kila mmoja ni balozi naamini hali hii itasambaa Tanzania nzima siku
chache zijazo," amesema.
Mtaalam
huyo amesema kitendo cha kumpa matumaini mwananchi kuwa atanufaika na
misitu yake baada ya miaka zaidi 80 kinahitaji elimu hivyo anaamini
dhana hiyo itasambaa nchini.
Korkonen
amesema Tanzania ina misitu mingi ya asili ambayo ikitunzwa kwa mfumo
wa kunufaisha wananchi itakuwa endelevu na salama.
No comments:
Post a Comment