Mtaribu wa FORVAC Kitaifa Emmanuel Msoffe akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kuwepo mashine za kuchakata mbao ambazo zinasaidia asilimia nyingi ya mbao kubaki na kuingiza sokoni.
Wajumbe wa Kamati ya Maliasili kijiji cha Sautimoja wakipasua gogo kwa kutumia mashine ya kisasa waliyonunuliwa na WWF.
SULEIMAN MSUYA, TUNDURU
USIMAMIZI
Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ), katika Msitu wa Chihuruka Kijiji
cha Sautimoja, Kata ya Namakambale Tarafa ya Nakapanya wilayani Tunduru
mkoani Ruvuma umerejesha mfumo wa elimu kijijini hapo kuwa kama wa
wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Itakumbukwa
wakati wa uongozi wa Hayati Nyerere elimu ilikuwa bure kwa asilimia 100
kuanzia elimu ya msingi jambo ambalo linatekelezwa Sautimoja kupitia
USMJ chini ya ufadhili wa Shirika la Mpingo na Maendeleo (MCDI) na
Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira na Wanyamapori Duniani
(WWF)
Akitoa taarifa ya
namna kijiji kinanufaika na USMJ mbele ya waandishi wa habari waliopo
katika ziara ya siku saba iliyoratibiwa na Program ya Mnyororo wa
Thamani wa Mazao ya Misitu (FORVAC), Mtendaji wa kijiji hicho Philemon
Dastan amesema mafanikio ni mengi ila hili la elimu ni kubwa zaidi.
Dastan amesema msitu wa kijiji umefanikiwa kuingiza zaidi ya shilingi 118.5 kwa kuuza magogo, mbao na mianzi.
Amesema
Msitu wa Chihuruka wenye ukimbwa hekta 21,969 umetengwa kwa ushirikiano
kati ya Halmashauri ya Tunduru, MCDI na WWF mwaka 2014.
"Sisi
msitu umeturejesha enzi za Mwalimu Nyerere katika elimu kwani tumuweza
kuwanunulia wanafunzi kalamu, madaftari, chaki na kujenga darasa hali
ambayo ilitokea wakati wa uongozi wa Nyerere.
Kupitia
mfumo huo wa kuwapatia mahitaji muhimu wanafunzi ufaulu umeongezeka
kutoka asilimia 80 hadi 92 hivyo USMJ unapewa kipaumbele Sautimoja,"
amesema.
Mtendaji amesema motisha hiyo imesaidia mahudhurio kuongezeka jambo ambalo linasababisha dhana ya elimu bure kivitendo.
Aidha
amesema shilingi milioni 118 zilizopatikana zimezesha kununua pikipiki
mbili, kujenga ofisi ya kijiji kwa shilingi milioni 26, kununua thamani
za ofisi, kufatua tofali za nyumba ya mtendaji, kununua vifaa vya doria
na kulipa bima ya afya kwa wajumbe 17 wa kamati ya maliasili.
Aidha, amesema katika kuhakikisha wanavijiji wanazidi kunufaika na USMJ wanatarajia kukata bima kaya zote 250.
"Kila
kaya moja itagharimu kiasi cha shilingi 30,000 ambapo itawezesha watu
sita kupata kadi za bima ya afya kwa wanakijiji 513,"amesema.
"Kama
tunavyojua kwamba ugonjwa ni jambo la dharura hivyo kwa wananchi kupata
kadi za CHF watakuwa na uhakika wa matibabu nyakati zote tumeona
mafanikio kwa kaya zile wanazotoka wajumbe wa kamati ya maliasili na
sasa tunaelekea kwa kijiji chote,"amesema.
Aidha amesema kijiji kina zaidi ya shilingi milioni 28 ambazo zitatumika kujenga zahanati ya kijiji.
"Kadi
tumepata lakini kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha tunajenga zahanati
yetu hapa kijijini ili kupunguza adha ya kwenda wilaya nyingine ya
Nanyumbu kufuata huduma afya,"amesema.
Aidha,
Dastan amesema pamoja na mafanikio waliyopata kuna changamoto ya mifugo
kuingia msituni, kukosa soko la uhakika wa mazoa ya misitu kama mbao
hivyo wameomba wafanyabishara kuja Sautimoja kununua mbao nzuri.
"Changamoto
ya soko tunaendelea kuipigania ni imani yangu ujio wenu utatangaza
fursa hii muhimu kuwa tuna mbao nzuri zinachanwa na mashine ya kisiasa,"
amesema.
Hadija Athuman
Katibu wa Kamati ya Maliasili amesema awali mradi ulikuwa na changamoto
ila kupatikana kwa mashine ya kuchakata mbao wameanza kunufaika.
Amesema
USMJ imechochea usawa wa kijinsia jambo ambalo awali halikuwepo huku
akiwasisitiza wakina mama kushiriki katika uhifadhi.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Sautimoja, Said Juma amesema miaka sita ya mradi
umerahisisha utendaji wenye kufuata misingi ya utawala bora.
"MCDI
na WWF wamechochea uwazi, uwajibikaji na utawala bora na kijiji
kimepata mafanikio makubwa ya maendeleo. Lakini pia ajira zimepatikana
kwa kijiji chote kushiriki kwenye USMJ," amesema.
Juma amesema mafanikio ambayo yamepatikana kupitia miradi ya USMJ imeweza kuunganisha familia na sio kutenganisha.
Naye
Shakila Bushiri amesema kuwa kimsingi wametambua umuhimu wa kutunza
misitu kwa maslahi ya maendeleo ya kikazi cha sasa na kijacho.
"Uhifadhi
umetukomboa sisi wanawake wa Kijiji cha Sautimoja maana fedha zote
zinazopatikana zinafanya shughuli za maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na
Kijiji kwa ujumla," amesema.
Samson
Remmy Kaimu Ofisa Misitu wilaya ya Tunduru amesema serikali ipo pamoja
na vijiji vinavyotekeleza miradi ya USMJ kwa kuwa ina manufaa kwa
wananchi, vijiji na nchi kwa ujumla.
Remmy
amesema wanaomba wadau wote wa misitu kuendelea kuibua miradi chanya na
wao watawaunga mkono na kwamba watawapa ushirikiano.
Kaimu
ofisa misitu huyo amesema hali ya uharibifu wa misitu katika vijiji
visivyo na USMJ ni kubwa tofauti na ile vyenye USMJ na kuwataka
wanavijiji kuhifadhi.
"Naomba
Serikali kuungana na wadau wote wenye miradi ya USMJ kama FORVAC, MDCI,
WWF, MJUMITA, TFCG na wengine huku akisisitiza elimu itolewe zaidi.
Marcel
Mutunda ambaye ni Mratibu wa FORVAC) mkoa wa Ruvuma amesema program
hiyo wamekuja nayo kuhakikisha misitu inakuwa salama lakini wananchi nao
wanufaike kiuchumi, kijamii na maendeleo.
Mutunda
amesema mradi huo ambao upo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii,
kupitia Idara ya Misitu na Nyuki kwa ufadhili wa serikali ya Finland
umekuwa ni chachu ya maendeleo kwa jamii na hata kuwafanya wananchi
kutambua thamani ya misitu.
Msimamizi
na Mtaalam wa Misitu FORVAC Alex Njahan amesema wamedhamiria kutoa
elimu kwa kina ili thamani ya mazao ya misitu nchini ionekane kuanzia
ngazi ya chini hadi juu.
Njahani
amesema program hiyo inatekelezwa kwenye wilaya 12 za Songea, Mbinga,
Nyasa, Namtumbo, Tunduru, Liwale, Ruangwa, Nachingwea, Handeni, Lindi,
Mpwapwa na Kiteto.
Mratibu
wa FORVAC Kitaifa, Emmanuel Msoffe amewataka waandishi wa habari nchini
kutumia kalamu zao vizuri kuelezea kwa kina faida za USMJ ili wafanya
maamuzi wapate uelewa.
Msoffe
amesema dhana ya USMJ bado haijaeleweka kwa kina hasa kwa wafanya
maamuzi hivyo ushahidi utakaonekana kupitia kalamu zao utawabadilisha.
"Mnapaswa
kutumia nafasi yenu kuiambia jamii kuwa misitu sio kuhifadhi pekee bali
inapaswa kutumika kuchochea mabadiliko ya kiuchumi, kijamii na
maendeleo kwa wanavijiji," amesema.
No comments:
Post a Comment